Skip to main content

BODI YA TMA YAFANYA ZIARA YA KIKAZI RADA YA HALI YA HEWA BANGULO,PUGU NA KITUO CHA HALI YA HEWA JNIA


Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imefanya ziara ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Mamlaka katika kituo cha Rada ya Hali ya Hewa, Bangulo, Pugu na Ofisi za TMA zilizopo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 23 Julai 2025.Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari na Makamu Mwenyekiti, Dkt. Emmanuel Mpeta.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Jaji Mshibe alisema lengo la ziara ni kukagua  na kutathmini usimamzi na utendaji kazi wa miundombinu ya TMA  na kutathmini  utekelezaji wa Maagizo na Maelekezo ya Bodi katika kuboresha huduma na pia kutambua changamoto zilizopo,  na kuona Taasisi ilipo na inapoelekea. “Bodi imekuwa ikitoa maelekezo hivyo leo ilikuwa ni siku maalum kuangalia utekelezaji wake”.Alisema Jaji Mshibe.

Alisisitiza kuwa TMA ya sasa imepiga hatua kubwa katika uboreshaji wa miundombinu ya utoaji huduma. Aidha, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka kwa miundombinu ya kisasa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na  Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Mabadiliko ya Tabianchi Dkt, Ladislaus Chang’a aliishukuru Bodi kwa kutembelea  na kujionea utendaji kazi wa Mamlaka katika  Uangazi, Uchakataji wa data na utoaji wa utabiri na kujionea miundombinu ya Kisasa ambayo Serikali imeiwezesha TMA kuipata. Pia alishukuru Bodi  kwa maelekezo ambayo wamekuwa wakiyatoa kupitia vikao mbalimbali vya bodi, na kuiwezesha TMA kuendelea kuwa bora.

Akitoa ufafanuzi wa faida za uwekezaji wa miundombinu ya kisasa katika sekta ya hali ya hewa nchini alisema “ Kupitia rada za hali ya hewa, Mamlaka imefanikiwa kuboresha utabiri wa hali ya hewa pamoja na kuendesha mafunzo ya rada kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati,  wataalamu wa hali ya  hewa kutoka nchi 10 za  Afrika Mashariki na Kati walipata mafunzo mjini Mwanza , Tanzania na  kuendelea  kuipa heshima kubwa nchi yetu”. 

Aliongeza kwa kufafanua kuwa, Serikali imeendelea kuhakikisha usimamizi wa mitambo hii ya kisasa inakuwa endelevu kwa kuajiri na kuwezesha wataalamu kupata mafuzo husika, ambapo mpaka sasa TMA ina  wahandisi 30.

Katika hatua nyingine wajumbe wa Bodi walipata fursa ya kutembelea Kompyuta Kubwa ya Kisasa (Computer Cluster) yenye uwezo mkubwa wa kuchambua na kuchakata taarifa za hali ya hewa na kuimarisha utoaji utabiri katika maeneo madogomadogo na mahsusi kwa haraka na usahihi zaidi. 

Imetolewa na;

KITENGO CHA MASOKO NA UHUSIANO,

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA).

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...