Skip to main content

MIKANDA NANE YA KIMATAIFA KUWANIWA JULAI 26, KNOCKOUT YA MAMA

 




Na Mwandishi wetu, Dar 

Pambano kubwa la Knockout ya mama msimu wa tano inatarajia kuwakutanisha mabondia wenye viwango vikubwa nchini Tanzania, Julai 26, 2025 katika  Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo kubwa litaweka historia kwa kuwa na mapambano nane ya kuwania mikanda mikubwa ya kimataifa ikiwemo ya WBO na WBC.

Akizungumza na waandishi wa habari  Julai 24, 2025 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Matangazo na Uzalishaji kutoka Kampuni ya Mafia Promotion Omari Clayton, amesema pambano hilo litakuwa na jumla ya mapambano 10 yakihusisha mabondia wa kimataifa.

"Mapambano nane yatakuwa ya mikanda na lengo ni kufanya "boxing" ya Tanzania iende mbali kimataifa, bondia atakayeshinda atapata fedha, mkanda na nyota, hivyo kutambulika kimataifa," amesema Clayton.

Ameongeza siku hiyo ya pambano itakuwa ni siku ya mtoko kwamba wanataka kila Mtanzania aweze kuifanya Julai 26, 2025 kuwa siku ya Mtoko kwa kwenda kushuhudia pambano hilo.

Naye, Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion Ally Zayumba akieleza maandalizi ya mwisho kuelekea usiku wa Knockout ya Mama Season 5, ameeleza kuwa kila kitu kipo tayari, na mashabiki wajiandae kushuhudia burudani ya kipekee isiyopimika.

Kwa upande wake, Promota Jay Msangi amewasifia  na kuipongeza Mafia boxing promotion kwa kuandaa pambano kubwa linalojulikana kama "Knock Out ya mama." 

Ameongeza kwa kusema kuwa uwekezaji waliouweka Mafia boxing promotion ni takribani bilioni mbili na ni uwekezaji mkubwa sana, kwamba  mapambano yanayokuja makubwa ya ubingwa ni WBC, WBO, na UBO yote yatafanyika nchini.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...