Skip to main content

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA 2025/26 KUKUSASANYA SHILL TRILL 2



Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imejiwekea lengo la kukusanya kiasi cha Sh2 trilioni kama mapato yasiyo yakikodi katika mwaka wa fedha 2025/26, imebainishwa.    

Hayo yalisemwa Jumatatu, Julai 28, 2025, na Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya siku nne kwa wakuu wa taasisi za umma yaliyoandaliwa na OMH kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi.

Kiasi kinachotarajiwa kukusanywa ni zaidi ya lengo la Sh1.6 trilioni ambalo serikali iliiwekea Ofisi ya Msajili wa Hazina kukusanya mwaka huu wa fedha.

“Ili tuweze kufikia lengo letu la kukusanya Sh2 trilioni itatubidi tuongeze bidii kwa asilimia 100 ya tulivyokuwa tunafanya mwaka wa fedha uliopita,” alisema Bw. Mchechu.

Katika mwaka wa fedha uliopita (2024/25) Ofisi ya Msajili wa Hazina ilikusanya kiasi cha Sh1.028 trilioni kama mapato yasiyo yakikodi.

Miongoni mwa vyanzo vikuu vya mapato yasiyo yakikodi ni Gawio---Mapato haya yanatokana na Mashirika na Taasisi zinazofanya biashara na yanakusanywa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni SURA 212 (Kifungu cha 180) na Sheria ya Mashirika ya Umma Sura 257 (Kifungu cha 15(2)(b)).  

Vyanzo vingine ni michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi--- Kifungu cha 12 (3) cha Sheria ya Fedha za Umma Sura 348 kinazitaka taasisi za umma (zisizo kwenye kundi la gawio) kuwasilisha asilimia kumi na tano ya mapato ghafi kwenda Mfuko Mkuu wa Serikali. 

Pia kuna mapato mengineyo ambayo huhusisha asilimia 70 ya mapato ya ziada ya taasisi za umma, marejesho ya mikopo na riba na mawasilisho yatokanayo na mtambo wa kuhakiki na kuwezesha mawasiliano (TTMS) kati ya Tanzania na nchi nyingine.

Msajili wa Hazina anaamini kuwa mafunzo elekezi kwa Kundi hili la pili linalojumuisha watendaji wakuu 114 wakiwemo walioteuliwa hivi karibuni pamoja na walioko katika nafasi zao kwa muda mrefu lakini hawakubahatika kupatiwa mafunzo, yatakuwa chichu ya mageuzi katika mashirika ya umma.

Lengo la mafunzo haya ni kuwaimarisha wakuu wa taasisi katika nyanja za uongozi na maadili, uwajibikaji wa kifedha na usimamizi wa uwekezaji wa umma ambao hadi kufikia mwaka 2023/24 umefikia takribani Sh86.25 trilioni, ambapo kiasi hiki kimewekezwa katika taasisi za umma 252 na kampuni ambazo Serikali ina hisa chache 56.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...