Skip to main content

RC CHALAMILA ASIKITISHWA NA HUDUMA MBOVU YA MABASI YAENDAYO HARAKA-DART







Asema Serikali sikivu ya Rais Dkt Samia Suluhu imesikia kilio hicho mwarobaini tayari umepatikana.

Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amefanya ziara katika Kituo cha mabasi yaendayo haraka DART kilichopo Kimara mwisho Wilaya ya Ubungo na kuitaka mamlaka inayosimamia mabasi yaendayo haraka UDART kuboresha huduma zao ili kumaliza adha wanayopitia wananchi wanaotumia usafiri huo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo RC Chalamila amesema hajaridhishwa na huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka kutokana na uchache wa mabasi jambo ambalo limekua likichangia huduma mbovu na kuwasababishia watumiaji wa usafiri huo adha kubwa  kinyume na dhamira ya Rais Dkt Samia ya kutaka kuboresha huduma yq usafiri katika Jiji hilo,hivyo ameitaka UDART kuboreha huduma.

Aidha RC Chalamila ametembelea upanuzi wa barabara ya Ubungo Kimara unaosimamiwa na TANROAD ambapo ameitaka mamlaka hiyo kumsimamia mkandarasi amalize ujenzi huo kwa wakati pia ameshauri uwepo wa huduma za vyoo kwenye maeneo ya vituo vikubwa ikiwemo kimara.

Katika hatua nyingine RC Chalamila ametembelea mamlaka ya kusimamia ujenzi wa barabara za mwendokasi DART iliyopo Ubungo maji jijini humo na kueleza mikakati ya Serikali chini ya Rais Dokta Samia kumaliza changamoto ya usafiri wa mwendokasi .

Aidha, kwa mradi wa kimara wamepata mwekezaji mpya anaitwa Trans Dar wakati kwa barabara ya Mbagala wamepata mwekezaji anaitwa Mophat wanaotarajia kuingiza magari yao hivi karibuni

Kwa upande wake, Menaja upangaji ratiba na udhibiti kutoka UDART Daniel Madilu amesema tayari wameshafanya tathmini ya changamoto ya usafiri huo na kwamba tayari wameagiza mabasi miamoja kutoka China yatakayoingia nchini mwezi wa tisa mwaka huu.

Naye, Mtendaji Mkuu wa DART  Dkt Othman Kiamia ameahidi kushughulikia changamoto zilizopo kwa sasa ili kuondoa kero kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kusimamia uingizaji mabasi yakutosha na yenye ubora kukidhi uhitaji wa huduma hiyo ya usafiri wa mwendokasi.


Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...