Skip to main content

HIFADHI YA MPANGA-KIPENGERE YAKONGA NYOYO ZA WALIMBWENDE MISS UNIVERSE 2025




Rais Samia Apongezwa uboreshaji Miundombinu

Na Beatus Maganja, Mbeya

Walimbwende wa Miss Universe Tanzania 2025 wametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na maono yake ya kukuza sekta ya utalii nchini kupitia maboresho ya miundombinu ya Hifadhi ya Mpanga Kipengere jambo linaloifanya Hifadhi hiyo kuwa kivutio kikubwa cha watalii nyanda za juu kusini.

Kauli hiyo imetolewa Agosti 29, 2025 na walimbwende hao mara baada ya  kufanya ziara maalum katika hifadhi hiyo iliyopo Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya ambayo inasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA ambapo walibaini fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia urithi wa asili wa eneo hilo.

"Tumeona historia ya Chifu Mkwawa, maji ya baraka na maajabu ya asili ya kipekee. Mpanga-Kipengere ni hazina ya Taifa letu. Sasa ni jukumu letu kama mabalozi kuutangaza urithi huu Kwa dunia nzima " alisema Nais Sayona ambaye ni mshindi wa Miss Universe Tanzania 2025.

Mbali na kukiri kujifunza mengi katika ziara hiyo, Mkurugenzi wa Mashindano hao nchini, Millen Happiness Magesa alisema mshindi wa shindano hilo atabeba kipande cha makala ya ziara hiyo na kukipeleka katika mashindano ya dunia yanayotarajiwa kufanyika Thailand huku akisisitiza kuwa hiyo ni nafasi ya kipekee ya kuitangaza Tanzania kupitia hifadhi hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Utalii Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ananias Lugendo alisema Serikali imewekeza katika maboresho ya miundombinu ya hifadhi hiyo ili kuifanya iweze kufikika kwa urahisi zaidi. Aliongeza kuwa uwepo wa mazao mengi ya kiutalii unachangia kuifanya  kuwa na mvuto wa kudumu mwaka mzima.

"Hifadhi hii inajivunia kuwa na zaidi ya maporomoko 53 yakiwemo aina 13 kati ya 14 zinazopatikana duniani ambapo maporomoko ya Kimani yamekuwa kivutio kikuu na sasa kupitia walimbwende hawa itapata hadhi ya kimataifa " alisema Lugendo.

Naye Afisa Utalii wa Hifadhi hiyo, Pendo Kimaro alisema ujio wa walimbwende hao ni hatua kubwa ya kuitangaza hifadhi hiyo Kimataifa kupitia majukwaa yao ya Kitaifa na Kimataifa.

"Tunataka ulimwengu ujue kuwa Tanzania ina maajabu, sio tu wanyamapori bali ina hazina ya kipekee yenye mvuto wa kiasili" alisema Kimaro.

Ziara hiyo ilifanyika kuanzia Agosti 27, 2025 ikihusisha walimbwende kumi bora wa Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2025 wakiongozwa na mshindi wa taji hilo Bi. Nais Sayona.

Washiriki hao walipata fursa ya kujionea vivutio mbalimbali vya hifadhi hiyo ikiwemo historia ya Chifu Mkwawa, bustani ya dunia, eneo la "massage" ya asili, tafakuri ya kina, matembezi ya mwituni, kuoga mvuke na maporomoko makubwa ya Kimani yenye urefu za zaidi ya mita 250.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...