Skip to main content

MKUTANO WA WAKUU WA TAASISI ZA UMMA KUCHOCHEA MAGEUZI NA USHINDANI

 


Na Mwandishi wetu

Katika kuendeleza juhudi za Serikali kuhakikisha taasisi za umma zinakuwa sehemu hai ya uchumi wa kisasa, Ofisi ya Msajili wa Hazina imeandaa kikao kazi maalum ‘CEO Forum 2025’ kitakachowaleta pamoja Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa mashirika ya umma nchini wapatao 700.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Agosti 23-26 jijini Arusha, unalenga kujadili kwa kina jinsi taasisi za umma zinavyoweza kuwa shindani katika soko la kimataifa, kuongeza mapato yasiyo ya kodi, na kushiriki kikamilifu katika kuendesha uchumi wa kisasa unaoongozwa na matokeo.

Kupitia mijadala ya kitaasisi, Serikali inalenga kuimarisha ufanisi, uwajibikaji na ubunifu katika taasisi hizi ili ziweze kuwa wabia halisi wa maendeleo ya Taifa. 

Aidha, akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumatatu, Agosti 11, 2025, Bi. Lightness Mauki, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini---Mashirika ya Umma ya kibiashara, alisema kipaumbele kitawekwa katika kufanikisha utekelezaji wa Dira 2050, kwa kuhakikisha taasisi za umma zinajipanga kuwa wabia wa kweli wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kwa mujibu wa Dira 2050, Serikali imedhamiria kuwa na uchumi wa kati wa juu ifikapo mwaka 2050, huku pato la Taifa likifikia $1 trilioni na pato la mtu mmoja mmoja $7000 kwa mwaka. 

Aidha, Mauki alisema ili kufikia matamanio hayo ni lazima kujenga misingi imara ya ushirikiano kati ya vyombo vya maamuzi na wasimamizi wa utekelezaji ndani ya taasisi za umma, ili kuongeza tija, uwajibikaji na uwezo wa kushindana katika mazingira ya kikanda na kimataifa.

Ni katika muktadha huo, katika kipindi ambacho dunia inakumbwa na mabadiliko ya haraka ya kiuchumi, kiteknolojia na kisera, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imetambua haja ya kuwa na jukwaa mahsusi la kujadili, kutathmini na kuimarisha mwelekeo wa pamoja wa taasisi zake za umma – ndipo likazaliwa wazo la CEO Forum miaka mitatu iliyopita.

“Serikali, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, inaendelea kuimarisha juhudi za mageuzi ndani ya taasisi za umma kwa kuandaa kikao kazi maalum – CEO Forum 2025 – ambacho kitawakutanisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wapatao 700 wa taasisi zote za umma nchini,” alisema Bi. Mauki.

Aliongeza: “Lengo letu kuu ni kutathmini kwa pamoja nafasi ya taasisi za umma katika uchumi wa sasa unaobadilika kwa kasi na kuhitaji mifumo shindani, bunifu na yenye uwajibikaji wa juu.”

Bi. Mauki alisema kwa mazingira hayo, watatumia mkutano huo kama jukwaa la kimkakati linalolenga kuimarisha mawasiliano, mshikamano wa kiutendaji, na kuweka dira ya pamoja kati ya bodi na menejimenti za taasisi za umma.

Alieleza kuwa mkutano huo si tu mkutano wa kawaida, bali ni sehemu ya mwendelezo wa mageuzi yanayolenga kuongeza mchango wa mashirika ya umma katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

“Tunatarajia majadiliano ya kina kuhusu namna taasisi zetu zinaweza kuwa shindani katika soko la kimataifa, ziweze kuongeza mapato yasiyo ya kodi, na kushiriki kikamilifu katika kuendesha uchumi wa kisasa,” alisema Bi. Mauki.

Aliongeza kuwa kaulimbiu ya mwaka huu, “Ushirikiano Endelevu wa Kibiashara Katika Mazingira Shindani Kimataifa – Nafasi ya Mashirika ya Umma,” inaonyesha wazi kwamba taasisi za umma haziwezi tena kujiendesha kwa mifumo ya zamani, bali zinahitaji mwelekeo mpya wa kibiashara, ushirikiano na ufanisi wa hali ya juu.

Katika kikao hicho, washiriki wanatarajiwa kujadili changamoto, fursa na mikakati ya mageuzi yenye kuleta matokeo.

Bi. Mauki ameweka bayana kuwa matarajio ya Serikali ni kuona mkutano huo unaleta matokeo, ikiwa ni pamoja na kubuni mifumo mipya ya usimamizi, kuimarisha maadili ya kiuongozi, na kujenga mazingira ya kazi yanayowezesha uwajibikaji na ubunifu.

Aliongeza kuwa kikao hicho pia kitaleta fursa ya kujifunza kutoka kwa taasisi zilizopiga hatua, na hivyo kutoa mwanga kwa zile zinazokabiliwa na changamoto.

Kwa msingi huo, Ofisi ya Msajili wa Hazina inatoa wito kwa wadau wote – ikiwemo sekta binafsi, vyombo vya habari, washirika wa maendeleo na wananchi kwa ujumla – kushiriki kwa njia mbalimbali katika kuunga mkono mkutano huo, ambao ni sehemu ya harakati za kitaifa za kujenga mashirika bora ya umma kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...