Skip to main content

TUKITUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA TUTAOKOA HEKTA 400,000 ZA MISITU ZINAZOTEKETEA KWA MWAKA-MJIOLOJIA NSAJIGWA






Awanoa Wanawawake na Wajasiriamali Songwe kuhusu Nishati Safi ya Kupikia

Atoa wito kwa Wadau kushirikiana na Wizara ya Nishati kutoa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia

Songwe

Imeelezwa  kuwa matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia si tu yanahatarisha afya bali pia yanachochea uharibifu wa mazingira ambapo takribani hekta 400,000 za misitu hupotea kila mwaka nchini kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa, jambo linalochangia kuongezeka kwa ukame na mabadiliko ya tabianchi.

Hivyo, Watanzania wameaswa kuhamia katika  matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi kama kuni na mkaa kutokana na athari zake kwa binadamu na mazingira.

Wito huo umetolewa leo Agosti 16, 2025, na Mjiolojia kutoka Wizara ya Nishati, Nsajigwa Maclean, wakati akitoa elimu ya  Nishati Safi ya Kupikia kwa  Wajasiriamali mkoani Songwe.

Amesema kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, ni asilimia 16 tu ya Watanzania ndio wanaotumia nishati safi ya kupikia, hivyo bado kuna magonjwa yanayotokana na moshi wa kuni na mkaa, ambayo yanasababisha vifo vya zaidi ya watu 33,000 kwa mwaka nchini.

atika ngazi ya kimataifa, amesema watu bilioni 2.1 hawana upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, huku zaidi ya watu milioni 3 wakifariki dunia kila mwaka kutokana na madhara ya kiafya yanayotokana na nishati isiyo safi ya kupikia ambapo  Kusini mwa Jangwa la Sahara zaidi ya watu milioni 960 hawana nishati hiyo.

Aidha amebainisha kuwa kuna dhana potofu miongoni mwa jamii kuwa chakula kinachopikwa kwa kutumia gesi au umeme hakiwi na ladha nzuri, jambo ambalo amesema halina msingi wa kisayansi na linaendelea kuwazuia wananchi wengi kufanya mabadiliko kuelekea matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Ameeleza kuwa Wizara ya Nishati imeweka mkakati wa kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ili kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia, huku mkakati huo ukiangazia mafanikio kutoka nchi nyingine kama India na Ghana, ambazo zimepiga hatua katika kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Imeelezwa pia kuwa changamoto kubwa kwa wananchi si kutotaka kutumia nishati safi ya kupikia bali wanahitaji elimu pia kuhusu matumizi ya nishati hiyo hivyo ametoa wito kwa Wadau kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Mkakati wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia. 

Katika semina hiyo wanawake na wajasiriamali walihimizwa kuwa mabalozi wa mabadiliko kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia si kwa ajili ya afya pekee, bali pia kwa ajili ya kulinda mazingira na kizazi kijacho.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...