Skip to main content

WAGOMBEA UDIWANI ILALA WATAKIWA KUVUNJA MAKUNDI

 



Na Mwandishi wetu 

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi amewaomba Wagombea wa Udiwani Kata zote waliyoteuliwa kugombea nafasi hiyo Wilayani humo,wakawe sehemu ya kuvunja makundi kati yao na kamati za siasa za kata,nakuondoa tofauti walizo nazo ili waingie kwenye uchaguzi wakiwa wamoja. 

Yared amewaasa Madiwani hao leo August 15,2025 wakati akiwakabidhi barua za uteuzi wa kugombea nafasi hiyo,nakuwasisitiza kuwa wamoja ili kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kupata Ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.

"Nimewatoa wasiwasi kuwa chama Cha Mapinduzi kimetumia Vigezo Mbalimbali ambapo kimebaini wanastahili na kufaa kugombea nafasi ya udiwani,walikua wagombea wengi lakini nafasi ilikua ni moja kwa maana hiyo waliopata nafasi ya uteuzi nimewaasa wasijione wao ni bora zaidi kuliko wenzao."

Ameongeza" Cha pili ambacho nimewaasa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi nafasi ya udiwani Wilaya ya Ilala,nimewaomba warudi chini wakajishushe kwa wale waliogombea nao na wanachama,wasipandishe mabega na kujiona wao ni wajanja sana kwa nafasi waliyoteuliwa bali ni nafasi ambayo imewangukia wao kwa wakati huu. 

Aidha Yared amesema kuwa wagombea hao wamekiri pasina shaka watakua bega kwa bega na viongozi wenzao,na wanakwenda kuvunja makundi,kuongoe na wapambe wao,na wafuasi wao, namna ya kuacha kurushiana maneno ya kejeri bali wataenda kukaa nakuunganisha timu zote ili chama Cha Mapinduzi kitoke kikiwa umoja kuanzia kwenye mchakato mzima wa kampeni za Uchaguzi ambazo zinatarajiwa kuanza August 28,Mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...