Skip to main content

WAZIRI MKUU: RAIS SAMIA AMEIHESHIMISHA TANZANIA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA


Aipongeza REA Kwa Kusimamia vyema utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi na Usambazaji umeme Vijijini

Awasisitiza Watanzania kushiriki Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia

Ataja faida za kutumia Nishati Safi ya Kupikia

Asema Serikali itaendelea kuwezesha wadau wa Nishati Safi ya Kupikia

Atoa wito kwa Sekta Binafsi kushiriki kikamilifu kwenye Kampeni ya Nishati Safi

Kilimanjaro

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameeleza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipa heshima nchi kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia inayopewa kipaumbele katika mataifa mengi duniani.

Amebainisha hayo Mkoani Kilimanjaro leo Agosti 30, 2025 alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya Uzinduzi wa Mpango wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Jeshi la Magereza iliyofanyika katika Gereza la Karanga na kuhusisha taasisi na wadau mbalimbali wa Nishati Safi ya Kupikia.

Amesema Rais Samia ni kinara wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati zisizo safi na salama na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia.

Amesema matumizi ya nishati zisizo safi zinamadhara kwa afya ya binaadamu kupitia joto na moshi unaotokana na nishati hizo ambao unatoa kemikali ambayo sio salama kwa afya hivyo kila mmoja abadilike na amhamasishe mwingine katika hilo.

"Rais Samia ametuonyesha njia ni muhimu tukahamasika na kuachana na matumizi ya nishati zisizo salama, tangu tumeanza 2024 takwimu zinaonyesha Jeshi la Magereza lilikuwa likikata mamia ya miti na limekuwa likipata usumbufu kupata kuni za kupikia; kwa kampeni hii misitu yetu inakwenda kusalimika lakini pia afya za wananchi zinanusurika," amesisitiza Mhe. Majaliwa.

Alibainisha kuwa hapo awali kabla ya kuanza kutumia Nishati Safi ya Kupikia, Jeshi la Magereza  lilikuwa likitumia zaidi ya tani mia kwa mwaka na sasa baada ya kuanza kutumia Nishati Safi ya Kupikia imewasaidia kupunguza gharama kwa zaidi ya 50%.

"Tunataka ifikapo mwaka 2034; 80% ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ya Kupikia, kwa manufaa yao na vizazi vijavyo," amesisitiza Mhe. Majaliwa. 

Vilevile, Mhe. Kassim Majaliwa ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi kubwa inayofanya ya kuwezesha na kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na kusambaza umeme vijijini na sasa vitongojini.

"REA imefanya kazi kubwa  ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia lakini pia katika suala la kusambaza umeme, imekamilisha kusambaza umeme vijijini na sasa inasambaza vitongojini, hongereni sana," amepongeza Mhe. Majaliwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amesema kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza wameendelea kujenga miundombinu ya nishati safi ya kupikia ili kuhamasisha matumizi hayo katika taasisi hiyo.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Katungu ameishukuru Serikali kwa kuliwezesha Jeshi la Magereza kuweza kutumia nishati safi ya kupikia katika magereza yote nchini na kuipongeza REA kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. 

"Hii yote ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100 zihame kutoka katika matumizi ya nishati chafu na kuhamia katika nishati safi ya kupikia, " Ameongeza CGP Katungu.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...