Skip to main content

NITALIPIA UPYA MIKATABA YA MADINI ILI WANANCHI WANUFAIKE - DOYO



Monduli, Arusha

Mgombea urais kupitia Chama cha NLD, Mhe. Doyo Hassan Doyo, ameendelea na ziara zake za kampeni zinazofanyika kwa mfumo wa kufikia na kuwafata wapiga kura popote walipo, kwa mtindo wa kampeni za kijiji kwa kijiji na kata kwa kata.

Akiwa njiani kuelekea Arusha, Mhe. Doyo alipita Kata ya Makuyuni, lakini pia alizungumza na wananchi wa Kata ya Meserani, Wilaya ya Monduli. Katika hotuba yake, aliwaeleza wananchi kuwa mikataba ya madini iliyosainiwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi imekuwa ikifanyika kwa usiri mkubwa, bila Watanzania kuonyeshwa manufaa wanayoyapata kutokana na mikataba hiyo.

Mhe. Doyo aliahidi kuwa, endapo atachaguliwa kuwa Rais, hatua yake ya kwanza itakuwa ni kuhakikisha anapitia upya mikataba ya madini ili kubaini kwa uwazi kile ambacho taifa linanufaika nacho. Alisisitiza kuwa suala hilo limekuwa siri kwa muda mrefu, jambo ambalo atalivalia njuga ili kuhakikisha rasilimali za Watanzania zinabaki salama na zenye manufaa kwa wananchi.

Aidha, aliwaambia wananchi hao kuwa wanaishi jirani na Mkoa wa Manyara, hususan Wilaya ya Simanjiro, ambako kuna biashara kubwa ya madini adimu duniani, yakiwemo madini ya Tanzanite. Hata hivyo, licha ya utajiri huo mkubwa, wananchi wa maeneo ya jirani hawajanufaika ipasavyo na rasilimali hizo.

“Nimepita Makuyuni, nikawakuta ndugu zenu wakiuza pakiti za miwa na kina mama wakiuza bagia. Nikajiuliza, inaingiaje akilini kuona Watanzania wanaoishi maeneo yenye migodi ya madini ya kipekee duniani bado wakiendelea kuuza vipande vya miwa baada ya miaka 60 ya uhuru? aingii akilini,” alisema Mhe. Doyo.

Mgombea huyo amewaahidi wananchi hao kuwa, endapo watamchagua, serikali yake itajenga viwanda vya kuongeza thamani ya madini ili wananchi wa ukanda huo wapate ajira zenye staha, badala ya kuendelea kujihusisha na biashara ndogo ndogo zisizo na tija, huku wakiishi karibu na utajiri mkubwa wa Tanzanite, madini yanaolitambulisha taifa lao duniani.

Kwa sasa, msafara wa mgombea urais huyo wa Chama cha NLD, unaelekea Arusha, Mara, Mwanza.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...