Skip to main content

SERIKALI YA AUSTRIA KUFADHILI MIRADI YA UMEME TANZANIA

 


Ni inayozalisha umeme kutokana na Jua; Takataka

Ufadhili huo ni kupitia Benki ya UniCredit ya Austria

Serikali ya Tanzania yaahidi ushirikiano

Serikali ya Austria kupitia Benki ya UniCredit  imeahidi kuipatia fedha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi cha Euro Milioni 20 sawa na takribani Shilingi bilioni 60 kwa ajili ya Utekelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia jua na takataka.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Merl Solar Technologies GmbH, Mha. Hannnes Merl alipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba Septemba 17, 2025 pembeni ya  Mkutano Mkuu wa 69 wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomic unaoendela Jijini Vienna, Austria.

Ili kuanza utekelezaji wa miradi hiyo, Mhandisi Mramba  ameikaribisha kampuni hiyo nchini Tanzania ili kukutana na wataalam na kuanza  kufanya maandilizi stahiki ya miradi hiyo mipya ya kuzalisha umeme  huku akiahidi kutoa ushirikiano katika kufanikisha Utekelezaji wa miradi hiyo.

Mha. Felchesmi Mramba ameeleza kuwa kampuni ya Merl  imeshatekeleza miradi mbalimbali ya umeme wa jua nchini akisema “kampuni hii imetekeleza  miradi ya umeme katika vijiji kumi (10) katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2017”.

Ametaja miradi hiyo kuwa  ni ya makontena 14 ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua katika Wilaya za Kongwa  mkoani Dodoma, Mlele mkoani Katavi, pamoja na Uyui mkoani Tabora ambapo mradi huo uligharimu kiasi cha  shilingi bilioni 16.2.

Ameongeza kuwa miradi hiyo imewezdsha kuzipatia umeme nyumba na makazi 812, nyumba za Ibada 27, Shule 6 na Vituo vya Afya 8.

Mha. Mramba ameishukuru Serikali ya Austria kwa kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi pamoja na nia ya Serikali ya Austria kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa Mkakati Mahususi wa Nishati (National Energy Compact) unaolenga kupeleka umeme kwa watanzania wote ifikapo mwaka 2030 kupitia mpango wa misheni 300.

Kikao kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Kampuni ya Merl kimefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Mjini Vienna nchini Austria na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania na Mwakilishi wa Kudumu nchini Austria Balozi. Naimi S. Aziz pamoja na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu,  Mha. Innocent Luoga.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...