Skip to main content

TATHMINI YA MCHANGO WA WANAHABARI YAONESHA KURIDHISHWA NA USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekutana na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini ili kujadili utabiri wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba – Desemba) 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Usafirishaji (NIT). Akizungumza wakati wa mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a alisema kupitia warsha hizi uelewa wa wanahabari kuhusu masuala ya hali ya hewa umeendelea kuimarishwa kwa kiasi kikubwa na hivyo kuwezesha taarifa zitolewazo na mamlaka kufikia jamii kwa urahisi na kwa wakati.

“Mnamo mwezi Julai mwaka 2025, Mamlaka iliandaa Dodoso maalumu kwa wanahabari ili kufanya tathmini ya utendaji kazi wake kwa Tasnia ya Habari, ambapo kwa taarifa niliyonayo ni kwamba tathmini hiyo imekamilika na matokeo yake yanaonesha asilimia 95 ya wanahabari waliotoa maoni yao wameridhishwa na usahihi wa utabiri wetu na asilimia 96.3 wameonesha kuzielewa taarifa hizo zinazotolewa na TMA hivyo kuzifikisha kwa jamii kwa lugha rahisi”. Alisema Dkt. Chang’a.

Aidha, Dkt. Chang’a ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wadau wa Maendeleo kwa kuendelea na uwekezaji katika miundombinu ya hali ya hewa nchini na hivyo kuwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa kuendelea kuboresha huduma zake kwa kutoa utabiri mahususi kwa sekta mbalimbali nchini.

“Kwa kuzingatia umuhimu wa huduma za hali ya hewa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuboresha miundombinu ya utoaji huduma za hali ya hewa ikiwemo ufungaji wa Rada za hali ya hewa na kuwajengea uwezo wataalam wa hali ya hewa, ambapo watumishi wapatao 97 wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wanaendelea na masomo ya elimu ya juu ndani na nje ya nchi”. Alisema Dkt. Chang’a

Naye, mwanahabari kutoka Harvest FM, Bw. Yonna Mgaya alitoa mrejesho wa namna taarifa za hali ya hewa zimekuwa rahisi kupatikana kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kufanikiwa kuzirusha zaidi ya mara mbili kwenye kituo chao. TMA inatarajia kutoa rasmi utabiri wa Msimu wa Mvua za Vuli 2025, tarehe 11 Septemba 2025, katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...