Skip to main content

TMA YAHIMIZWA KUENDELEA KUSHIRIKISHA WADAU ILI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA


Dodoma

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imehimizwa kuendelea kushirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa nchini. Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari alisema hayo wakati akifungua mkutano wa 24 wa wadau katika kujadili Utabiri wa Msimu wa Mvua za Vuli (Oktoba hadi Disemba) 2025, wenye kaulimbiu “matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika kupanga na kutekeleza majukumu ya kila siku kwa maendeleo endelevu” uliofanyika kwenye ukumbi wa PSSSF, jijini Dodoma, tarehe 08/09/2025.

“Tunapoelekea kutoa Utabiri wa Mvua za Vuli (Oktoba hadi Disemba), 2025 napenda kuipongeza TMA na kuwahimiza kuendeleza utaratibu huu wa kuwashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali katika hatua za maandalizi ya utoaji wa utabiri wa mvua za misimu hapa nchini. Ushirikiano huu ni mfano wa kuigwa na unafaa kuendelezwa hasa katika kipindi hiki ambacho Dunia inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.” Alisema Jaji Mshibe. 

Aidha, Jaji Mshibe aliwasisitiza TMA kuhakikisha taarifa zinatoka mapema kama inavyostahiki kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano. “Ulimwengu wa sasa upo kiganjani”. Aliongezea Jaji Mshibe.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) Dkt. Ladislaus Chang’a alielezea umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau kutoka sekta mbalimbali katika utoaji wa huduma za hali ya hewa ambao umesaidia kuimarisha utoaji wa huduma za hali ya hewa na kuchochea matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa kwa jamii.

Wakitoa mrejesho wa athari za Mvua za Masika 2025 katika sekta zao, Mdau kutoka sekta ya kilimo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Bw. Wilfred Kavishe aliipongeza TMA kwa kutoa taarifa sahihi zilizosaidia upangaji  wa malengo ya mkoa katika uzalishaji, aliongezea kwa kusema kuwa Msimu wa Mvua za Masika 2025 Sekta ya Kilimo iliathirika kwa kiwango kikubwa hasa kwa wakulima ambao hawakufuata ushauri wa kitaalamu hali iliyopelekea malengo ya uzalishaji kuwa chini ya wastani ya matarajio yao. 

Naye mwakilishi wa wadau kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu wa Maafa) Bw. Emmanuel Lyimo alieleza namna taarifa za awali za mvua za Masika 2025 zilivyosaidia katika kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuziandikia wizara, Mamlaka za Mikoa, kuandaa mkakati wa kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea, kutoa mafunzo pamoja na kuandaa mpango wa dharura  kwa maeneo yaliyotarajiwa kuathirika. 

Kupitia mkutano huo, wadau walielezwa tathmini ya utabiri wa Mvua za MASIKA (Machi hadi Mei) kwa mwaka 2025 ulikuwa sahihi kwa 87.5%, huku TMA ikitarajia kutoa rasmi utabiri wa Msimu wa Mvua za Vuli 2025 tarehe 11 Septemba 2025, Jijini Dar es salaam.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...