Skip to main content

WASIRA: TUTAENDELEA KULINDA AMANI KWA MAENDELEO YA WATANZANIA

 




Na Mwandishi Wetu,  Kisarawe

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kulinda amani, umoja na mshikamano kwa kuwa bado hakijakamilisha lengo la kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo makubwa zaidi.

CCM imesema jukumu la kulinda amani umoja, mshikamano na kuleta maendeleo makubwa ya Tanzania imelirithi kutoka kwa vyama vya ukombozi Tanu na Afro Shiraz, hivyo itaendelea kulilinda kwa wivu mkubwa.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,  Stephen Wasira alieleza hayo jana, Kisarawe mkoani Pwani alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Pwani akiwa katika ziara ya kumwombea kura mgombea urais wa CCM Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea ubunge na udiwani waliosimamishwa na Chama kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

"CCM imekabidhiwa jukumu la kuendeleza umoja, mtu akijaribu kuvunja umoja anavunja msingi tuliokabidhiwa, CCM hatuwezi kuwa miongoni mwa wale wanaounga mkono wanaotaka kuvunja umoja wa nchi, ni kazi tulikabidhiwa, ya historia," alisema.

Mbali na hlio, alisema kazi ya pili ambayo CCM imekabidhiwa na inaendelea kuisimamia ni kuhakikisha amani inaendelea kudumu.

"Msingi wa amani ni umoja mkivunja umoja amani inakwisha, ndiyo, amani, amani ni kitu muhimu lakini ukikizoea unaweza kuona ni bure kama hewa maana hewa unaihitaji zaidi unapokaribia kufa ndipo unasema leteni mashine tuongeze hewa, lakini hii ya sasa bure tu unafikiri ni sawa inapatikana haina tabu, lakini amani ikitoweka haiwezi kurudi na waliokwisha onja ukosefu wa amani wanajua na msingi mkubwa ni ubaguzi.

"Wanagombana kwa makabila yao, wanagombana kwa dini zao, halafu amani inatoweka, ni matatizo madogo madogo sana lakini gharama yake ni kubwa," alieleza.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...