Skip to main content

BRELA, MORUWASA Waipongeza TANESCO Mageuzi ya TEHAMA




Ni kutokana na mabadiliko ya kidijitali katika utoaji wa huduma kwa Wateja

Waahidi kuongeza ufanisi katika Taasisi zao kupitia mafunzo waliyoyapata

Na Josephine Maxime, Dar es Salaam

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepongezwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kwa uwekezaji wake mkubwa katika teknolojia ya mawasiliano ambao umeimarisha kwa kiwango kikubwa huduma kwa wateja.

Pongezi hizo zimetolewa na viongozi wa Taasisi hizo baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika Kituo cha Huduma kwa Wateja cha TANESCO (Call Center), aambapo walishuhudia jinsi mifumo ya TEHAMA na huduma kwa wateja zinavyoshirikiana kutatua changamoto kwa haraka na kuongeza ufanisi.

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja TANESCO, Bi. Irene Gowelle, amesema TANESCO imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuboresha huduma kwa wateja hatua ambayo imechangiwa pia na uwekezaji uliofanyika  katika teknolojia.

“Tunaona matunda ya uwekezaji huu mkubwa uliofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati. Sasa taasisi nyingi zinakuja kujifunza kutoka kwetu, jambo ambalo awali halikuwepo. Lengo letu ni kuhakikisha kila mteja anapata majibu kwa haraka na changamoto zake zinatatuliwa kwa ufanisi,” alisema Bi. Gowelle.

Kwa upande wao, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa MORUWASA, Bw. Kiguhe Benno Lyang’onjo, na Afisa Habari Mkuu kutoka BRELA, Bi. Joyce Mgaya, wamesema wamevutiwa  na namna TANESCO ilivyowekeza katika mifumo ya mawasiliano, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza malalamiko ya wateja na kuongeza ufanisi wa huduma.

“TANESCO mmepiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia ya mawasiliano. Mafunzo haya yametupa mwanga wa namna bora ya kuimarisha huduma kwa wateja katika taasisi zetu. Tutayatumia kuleta mageuzi chanya,” alisema Bi. Mgaya.

Ziara hii ni sehemu ya utaratibu wa mashirika ya umma kushirikiana na kujifunza kutoka kwa wenzao waliopiga hatua katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji, ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...