Skip to main content

DALILI ZA UWEPO WA GESI ASILIA KATIKA KITALU CHA LINDI-MTWARA





Utafiti wa kina unaendelea katika Kitalu cha Lindi–Mtwara

Dkt. Mataragio akagua maendeleo ya mradi, aagiza ukamilike kwa wakati

Akagua pia mradi wa kuongeza uzalishaji wa gesi katika kitalu cha Mnazi Bay

RC Mtwara asema Gesi Asilia ni kichocheo cha wawekezaji mkoani

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanamawa asisitiza faida kwa jamii kupitia ajira na miundombinu

Utafiti unaoendelea kufanyika katika Kitalu cha Lindi–Mtwara, kinachojumuisha jumla ya vijiji 48 katika eneo la takriban kilomita za mraba 736 – vijiji 40 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara (Mtwara DC) na vijiji 8 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama (Mtama DC) – umeonesha dalili za uwepo wa Gesi Asilia, hususani katika vijiji vya Mnyundo na Mpapura, mkoani Mtwara, ambapo visima vya maji vilibainika kuvujisha gesi asilia.

Katika ziara yake ya kukagua miradi ya gesi na mafuta mkoani Mtwara, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, amesema kuwa utafiti wa awali unaonesha uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa gesi asilia katika eneo hilo.

“Kwa kutumia data za mitetemo zilizokusanywa awali, tumebaini kwamba kuna hadi asilimia 32 ya uwezekano wa gesi kuwepo katika kitalu hiki,” amesema Dkt. Mataragio.

Ameeleza kuwa mahitaji ya gesi yamekuwa yakiongezeka katika sekta mbalimbali zikiwemo viwanda, matumizi ya majumbani na usafirishaji – jambo linaloifanya Serikali kuendelea kuchochea utafutaji na uendelezaji wa vyanzo vya nishati hiyo ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Katika ziara hiyo, Dkt. Mataragio pia alitembelea mradi wa kuongeza uzalishaji wa gesi katika eneo la Mnazi Bay, ambapo amebaini kuwa mradi huo uko katika hatua ya maandalizi kwa asilimia 68.

Mradi wa Mnazi Bay unahusisha visima vitatu vya gesi asilia, ambapo serikali inatarajia kuongeza uzalishaji kwa wastani wa futi za ujazo milioni 45 kwa siku kutoka kwenye visima viwili, huku kisima kimoja kikiwa ni kwa ajili ya utafiti zaidi wa uwepo wa gesi katika eneo lingine katika kitalu.

Dkt. Mataragio ameliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilishwa kwa mujibu wa ratiba ilivyopangwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, amesema kuwa gesi asilia imekuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji mkoani humo, na kwamba uwepo wa miradi hiyo umechochea shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

“Kwetu sisi watu wa Mtwara, sekta ya nishati ni msingi wa maendeleo na usalama wetu. Nawapongeza TPDC na wadau wote kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya gesi asilia ambayo pia imetoa ajira kwa wakazi wetu,” amesema Kanali Sawala.

Mjiolojia Paschal Njiko, ambaye ni Mkurugenzi wa Utafutaji, Uendelezaji na Uzalishaji wa Mafuta na Gesi kutoka TPDC, amesema Shirika hilo litaendelea kusimamia wakandarasi kwa karibu ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na ndani ya bajeti.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanamawa, Bw. Selemani Hassani, ameishukuru Serikali kupitia TPDC kwa kuleta mradi huo kijijini kwao, na kueleza kuwa tayari wananchi wameanza kunufaika kupitia fursa za ajira na maboresho ya miundombinu.

“Kupitia mradi huu, tumepata barabara ndogondogo za mitaa ambazo zinarahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi. Wananchi pia wamepata kazi mbalimbali ambazo zimewawezesha kuongeza kipato,” amesema Mwenyekiti huyo.

Hadi sasa, zaidi ya ajira 1,200 za muda mfupi zimetolewa kwa wanachi wa Mtwara kupitia mradi wa kuchukua taarifa za mitetemo katika kitalu cha Lindi-Mtwara.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...