Skip to main content

DC WANGING'OMBE AFUNGA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA GHASIA KWA ASKARI WA TAWA







Aridhishwa na umahiri wa Askari hao

Na. Beatus Maganja, Njombe.

Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mhe. Zacharia Mwansasu, Oktoba 8, 2025 amefunga  rasmi mafunzo siku 10 ya kukabiliana na ghasia (Anti-Riot) kwa kikosi maalum cha Askari 60 wa mwitikio wa haraka wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA (RRT) katika Kituo cha Mafunzo cha Welela Mkoani Njombe, akisisitiza umuhimu wa nidhamu, weledi na uzingatiaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mhe. Mwansasu alisema "Serikali inatambua changamoto zinazowakabili Askari wa Uhifadhi, ikiwemo hatari wanazokutana nazo katika kulinda rasilimali za taifa, ambapo baadhi wamejeruhiwa na wengine kupoteza maisha." Na kuongeza kuwa mafunzo hayo yaliyotolewa na TAWA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi yatasaidia kuongeza ufanisi na uwezo wa askari kukabiliana na ghasia kwa kutumia nguvu ya kadiri bila kuathiri haki za binadamu.

Mhe. Mwansasu alieleza kuridhishwa na umahiri uliooneshwa na Askari hao katika mafunzo ya vitendo, yakiwemo matumizi ya mabomu ya machozi, upekuzi, ukamataji watuhumiwa na mazoezi ya ukakamavu. Alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kutoa mafunzo hayo na kuomba kuendeleza ushirikiano huo ili kuboresha utendaji wa Jeshi la Uhifadhi.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alitumia fursa hiyo kulaani vikali vitendo vya baadhi ya wananchi kuvamia na kuwashambulia Askari wa Uhifadhi wakiwa kazini. Aliwataka wananchi kuacha mara moja kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa na kuheshimu sheria za uhifadhi.

Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Mwansasu aliipongeza Menejimenti ya TAWA kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwataka wahitimu kutumia ujuzi walioupata kuboresha uhifadhi na kuongeza mapato kupitia utalii.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Uhifadhi – Huduma za Shirika, Thabit Maarufu, ambaye alimwakilisha Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha TAWA kifedha na kwa rasilimali watu, jambo linalozidi kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi nchini.

Aidha, Naibu Kamishna Maarufu alitoa shukrani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, kwa kuruhusu wataalamu wa jeshi hilo kushiriki katika kutoa mafunzo ya kukabiliana na ghasia kwa Askari wa Uhifadhi. Alisema ushirikiano huo ni kielelezo cha mshikamano wa taasisi za ulinzi na usalama katika kulinda rasilimali za taifa.

Akizungumzia mipango ya mbele, alibainisha kuwa TAWA imeandaa mpango maalumu wa kuboresha mfumo wa mafunzo kwa kuongeza kozi mbalimbali ikiwemo mafunzo ya uokoaji majini na kuogelea kwa askari wake, ili kuwaongezea uwezo wa kukabiliana na changamoto katika maeneo mbalimbali ya uhifadhi.

Vilevile, alisema mamlaka imepanga kuongeza vifaa, kuboresha miundombinu ya mafunzo, na kuhakikisha Kituo cha Mafunzo cha Welela kinajengewa uwezo wa kuwa kituo bora na cha mfano nchini katika kutoa mafunzo ya kiusalama na uhifadhi.

Naye Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi wa TAWA, Abraham Jullu, amelishukuru Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori Duniani (WCS) Kwa mchango wake mkubwa linalotoa Katika shughuli za uhifadhi nchini hususani uwezeshaji wa mafunzo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya RRT  yanayolenga kuimarisha uwezo na umahiri wa Askari hao katika utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi.

Aidha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Asel Mwampamba aliishukuru TAWA kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika kutoa mafunzo hayo, akisisitiza kuwa ushirikiano huo utaendelea kuimarisha nidhamu, ufanisi, na weledi katika utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi nchini.

Kadhalika, Mratibu wa ulinzi wa program ya Ruaha Katavi WCS  Bw. Stanley Mbilinyi alisema Shirika hilo linajivunia kushirikiana kwa ukaribu na TAWA katika kuanzisha na kuunga mkono vikosi vya kwanza vya RRT nchini Tanzania tangu mwaka 2015, pamoja na kushirikiana  na taasisi hiyo kuandaa nyaraka muhimu za mipango na kujenga uwezo wa kutekeleza mbinu hii kitaifa.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...