Skip to main content

KATIBU MKUU NISHATI AHIMIZA UZALENDO NA UADILIFU KWA WANACHAMA WA EWURA CCC

 



Azindua Baraza la Tatu la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba, ametoa wito kwa wajumbe wa Baraza jipya la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA Consumer Consultative Council – EWURA CCC) kuwa na nidhamu, uzalendo na uwajibikaji  katika majukumu yao, ili kuongeza ufanisi wa kazii na kuleta manufaa kwa wananchi.

Akizungumza jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la tatu la EWURA CCC pamoja na mafunzo kwa wajumbe wapya, Mha. Mramba amewahimiza wajumbe hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kuweka mbele maslahi ya taifa.

“Ni muhimu kila mjumbe kuwa mfano wa uwajibikaji na uadilifu. Baraza hili lina jukumu kubwa la kusikiliza na kuwasemea watumiaji wa huduma za nishati na maji, hivyo nidhamu na uzalendo ni nguzo kuu za mafanikio." Amesema Mhandisi Mramba

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa EWURA CCC, Bi. Stella Lupimo, alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wajumbe wapya ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, hususan katika kusimamia masuala yanayohusu haki na usalama wa watumiaji wa huduma hizo.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Poline Msuya, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wote wa sekta ya nishati ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora, nafuu na endelevu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji, Bw. Hassan Minga, aliahidi kuwa baraza hilo jipya litajikita zaidi katika kusikiliza changamoto za wananchi na kuzifikisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya utatuzi.

Uzinduzi wa baraza jipya la tatu la EWURA CCC na mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuimarisha uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika usimamizi wa sekta za nishati na maji, ili kuleta tija na maendeleo kwa jamii.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...