Skip to main content

MRADI WA TAZA KUFUNGUA SOKO JIPYA LA BIASHARA YA UMEME AFRIKA


Wafikia asilimia 83

Dkt. Mataragio akagua mradi na kutoa maelekezo TANESCO

TAZA kuunganisha Mkoa wa Rukwa na gridi ya Taifa

Kuimarisha upatikanaji umeme Mikoa ya Kusini mwa Tanzania

Mbeya

Imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Zambia kupitia Tunduma (TAZA) umefikia asilimia 83.45 huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Mei 2026 na hivyo  kufungua soko jipya la biashara ya umeme barani Afrika.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo leo Oktoba 23, 2025 katika eneo la Iganjo, Mbeya, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema mradi wa TAZA ni muhimu kwa Taifa kwa kuwa utaiunganisha Tanzania na Nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika (Southern Africa Power Pool) na pia kuimarisha muunganiko wa ukanda wa Mashariki mwa Afrika (East Africa Power Pool).

“Nimshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya nishati. Kupitia mradi huu tutaimarisha biashara ya kuuza na kununua umeme kati ya nchi za Mashariki mwa Afrika na zile zilizopo Kusini mwa Afrika”. Amesema Dkt. Mataragio

Kuhusu biashara ya umeme ya kikanda, Dkt. Mataragio amesema kuwa tayari Tanzania imeshaunganisha gridi ya umeme na  Nchi za Afrika za Kenya, Rwanda, Burundi na Ethiopia kupitia muunganiko wa East Africa Power Pool.

“Tutaunganisha pia gridi na nchi za Kaskazini na Magharibi mwa Afrika ili Afrika nzima tuweze kuuziana umeme ikiwa ni sehemu pia ya  kutekeleza Mpango wa Nishati unaolenga kuwafikishia umeme waafrika takribani milioni 600 ambao bado hawajafikiwa na nishati ya umeme”. Amesisitiza Dkt. Mataragio.

Kuhusu mradi wa TAZA, ameeleza kuwa unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ambao ni Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa Dola za kimarekani milioni 584.

Amesema kuwa mbali ya mradi wa TAZA kuunganisha gridi za umeme za Nchi za Kusini mwa Afrika, utauunganisha Mkoa wa Rukwa na umeme wa gridi pamoja na kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe.

Baada ya kukagua mradi huo, Dkt. Mataragio ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linamsimamia Mkandarasi kwa karibu hasa katika kipindi hiki cha mvua ili hatua za awali za ujenzi wa misingi (foundation) ziweze kukamilika kwa wakati na kumtaka Mkandarasi kuhakikisha vifaa vyote vipo eneo la Mradi.

Katika hatua nyingine Dkt. Mataragio ameiagiza TANESCO kuhakikisha inapeleka umeme eneo la Ngozi unapotekelezwa mradi wa kuzalisha umeme kwa jotoardhi ambapo kwa hivi sasa mitambo ya uhakiki wa jotoardhi katika eneo hilo inatumia mafuta ya dizeli.

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu aliambatana na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Innocent Luoga na watendaji wa Wizara ya Nishati na TANESCO.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...