Skip to main content

DKT. KIJAJI AIPA TANO BODI YA TAWA



Na, Sixmund Begashe, Arusha

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imepongezwa  kwa ubunifu wake katika utekelezaji wa majukumu yake  yaliyosababisha mafanikio katika uhifadhi na Utalii nchini. 

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, ametoa pongezi hizo leo Januari 08, 2026 Jijini Arusha wakati akipokea taarifa ya  utekelezaji kazi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA inayomaliza muda wake. 

Dkt. Kijaji amesema ubunifu katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo, umeendana sambamba na maono ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uhifadhi endelevu wa urithi wa  rasilimali kwa maslahi ya vizazi vijavyo na Taifa kwa ujumla. 

Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine, Bodi hiyo  imewezesha  kuongezeka kwa  wawekezaji na mapato kusababisha kuimarika kwa uhifadhi, kupungua kwa uvamizi katika maeneo ya hifadhi na mapori tengefu pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia licha ya uwepo wa maeneo ya maboresho.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Naibu Katibu wa Wizara hiyo Bw. Nkoba Mabula, amemuhakikishia Waziri Kijaji kuwa Ofisi yake itaifanyia kazi taarifa hiyo iliyo kabidhiwa ili kuongeza tija zaidi katika uhifadhi na Utalii kupitia TAWA na taasisi zingine za uhifadhi nchini.

Pamoja na kuushukuru uongozi wa Wizara kwa ushirikiano mkubwa,  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko  amesema mafanikio mengine ni  kuboresha mwitikio wa haraka katika matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu kupitia doria zinazohusisha vikosi maalum vya TAWA kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori wa vijij (VGS).

Pia aliongeza kuwa katika kipindi husika TAWA iliweza kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizp kutokana na usimamizi madhubuti wa mifumo ya udhibiti wa ndani (Internal Controls) na kushirikisha jamii katika uhifadhi kupitia miradi ya jamii, uvuvi na ufugaji nyiki Kupitia Hifadhi na kutoa gawio kwa wanufaika.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...