Skip to main content

TUNA DENI LA KUSIMAMIA MIRADI NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO YA KWELI–MHE. SALOME

 




Aanza ziara ya kikazi mkoani Shinyanga kukagua miradi ya nishati

Ataka changamoto za wananchi zitatuliwe kwa wakati

Siku 100 za Rais Samia Umeme kuwashwa kwenye vitongoji mkoani Shinyanga

SHINYANGA

Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa la kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo sambamba na kusikiliza pamoja  na kutatua kero za wananchi ili kufanikisha maendeleo ya kweli.

Mheshimiwa Salome ameyasema hayo leo tarehe 8 Januari, 2026, mkoani Shinyanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya nishati inayotekelezwa mkoani humo. 

Amesema wananchi wana imani kubwa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa viongozi kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinatatuliwa kwa wakati.

Ameongeza kuwa katika siku 100 za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Wizara ya Nishati imejipanga kuhakikisha umeme unawashwa kwenye miradi ya vitongoji mkoani Shinyanga ili kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Katika hatua nyingine,  Mheshimiwa Salome ametembelea Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, ambapo alikutana na Katibu wa CCM Mkoa huo pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) sambamba na Sekretarieti ya Mkoa ambapo amesema kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya Chama na Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake, Bi. Odilia Abraham Batimayo alisifu utendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na TANESCO kwa kushughulikia kero na changamoto za wananchi kwa wakati, hatua inayochangia kujenga imani kwa wananchi kwa Serikali yao.

Mheshimiwa Salome yuko mkoani Shinyanga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati, ikiwemo mradi wa umeme wa jua wa Kishapu pamoja na miradi ya umeme wa vitongoji katika vijiji mbalimbali 

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...