Skip to main content

DIWANI JESCA MAHMOUD MSOLLA AZINDUA KLINIKI YA VYETI VYA KUZALIWA BUYUNI

 


Na AyraNewstz

DIWANI wa kata ya Buyuni   Wilayani Ilala Mkoa Dar es Salaam, JESCA MAHMOUD MSOLLA, amezindua Kiliniki ya vyeti vya kuzaliwa kata ya Buyuni kwa ajili ya kuwasogezea wananchi huduma za kijamii karibu na makazi yao. 

Kampeni hiyo ya kutoa vyeti vya kuzaliwa  ambayo itakuwa wa siku kumi kutoa huduma ofisi za Afisa Mtendaji wa kata ya Buyuni ilianza Mei 13 itaendelea mpaka Mei 24 mwaka huu .

Akizungumza kwa niaba ya Diwani wa Buyuni, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Buyuni ,Sylvanus Benard Mwenda ,alisema zoezi hilo limeratibiwa na Diwani Jesca Mohmoud Msola kwa ajili ya kutatua kero za wananchi wake sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi  CCM .

"Diwani Jesca Mohmoud Msola, ameiona hii changamoto kubwa ya vyeti vya kuzaliwa ndio akabeba jukumu la kuleta RITA waweze kutoa vyeti vyeti vya kuzaliwa vinatolewa hapo hapo kwa gharama za Serikali "amesema Mwenda.

Mwenda amesema katika Jamii lazima uwe na vyeti vya kuzaliwa ili uweze kupata huduma nyingine ikiwemo kuomba Kitamburisho cha Taifa NIDA au hati ya kusafiria..

Aidha amesema zipo changamoto zingine shule na vyuoni wanafunzi wengi hawana vyeti hivyo kulazimika kupata usumbufu wa baadhi ya huduma.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na RITA kwa kusogeza huduma hiyo ya vyeti vya kuzaliwa .

Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni ya Kliniki ya Rita Wilayani Ilala Heri shaban amesema dhumuni la kupeleka huduma hiyo kusajiliwa wananchi vyeti vya kuzaliwa awali kulikuwa na Kliniki ya Vitamburisho vya TAIFA NIDA akakumbana na changamoto kubwa wananchi wengi vyeti vya kuzaliwa walikuwa hawana hivyo  ikapelekea kukosa fursa ya kupata NIDA ikalazimika kuomba maombi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuomba RITA wafike Kata za pembezoni kutoa hiduma .

Kwa upande wake Afisa Msajili wa Vyeti vya kuzaliwa Rita  ,Erasto wambura amesema dhumuni la kampeni hiyo kusaidia Serikali kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kuwa cheti cha kuzaliwa kinasaidia mambo mengi Kliniki ya Rita kwa sasa wameweka Kambi Buyuni,Chanika na Gongolamboto Ofisi za Serikali amewataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo. 

Afisa Wambura amesema dhumuni la Kliniki ya Rita kuwafikia watu wengi zaidi ,aliwataka wananchi kubeba nyaraka zote za muhimu ikiwemo taarifa za Wazazi,Tangazo,kadi ya mimba na kadi ya Kliniki au cheti cha ubatizo. 

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...