Skip to main content

TMA YAITAKA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI



Ayra Nwestz

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imeishauri jamii kuchukua hatua stahiki za kiafya ili kujikinga na magonjwa yanayoweza kusababishwa na mabadiliko hali ya hewa ya baridi na vumbi.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mwelekeo wa hali ya kipupwe katika kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti (JJA) mwaka huu.

Aidha Dkt. Chang'a pia amewashauri wafugaji kuendelea kuzingatia ratiba za kuogesha mifugo ili kudhibiti visumbufu na magonjwa pamoja na kufuata ushauri wa wataalamu, na maji na malisho yanapaswa kutumika kwa uangalifu ili kupunguza athari zinazotarajiwa.

Sambamba amewashauri wakulima kulima kwa kuzingatia ushauri wa maafisa ugani katika maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua katika kipindi hiki cha msimu wa kipupwe.

"Kwa watumiaji wa bahari, taarifa hii itasaidia kupunguza athari za upepo unaotarajiwa. Pia, sekta za ujenzi, madini na uchukuzi zinatarajiwa kunufaika kutokana na hali ya hewa inayotarajiwa," amesema.Aidha, ameendelea kusema kuwa taarifa hiyo watumiaji wengine wote waitumie ipasavyo na wanashauriwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa zikiwemo utabiri wa kila siku, angalizo na tahadhari ili kuongeza ufanisi na usalama wa shughuli zao.

Katika hatua nyingine, Dkt. Chang'a amesema kuwa kwa kawaida msimu wa kipupwe hutawaliwa na upepo wa kusini ambapo msimu wa kipupwe 2026 unatarajiwa kutawaliwa na upepo uliopungua nguvu kidogo kama ilivyo kawaida, utakaovuma kutoka kusini mashariki kwa maeneo mengi ya nchi, na vipindi vichache vya upepo mkali utakaovuma kutoka kusini hususan katika kipindi cha miezi ya Juni na Julai 2026 katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu.

Aidha, amesema kuwa kwa kawaida kipindi cha msimu wa kipupwe (JJA) hutawaliwa na hali ya ukavu katika maeneo mengi ya nchi, ambapo kwa JJA 2026, vipindi vya mvua za nje ya msimu vinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria hususan Mkoa wa Mara pamoja na ukanda wa pwani na maeneo ya nchi kavu (mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Mtwara, Lindi na Pwani ikijumuisha Kisiwa cha Mafia pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba) na sehemu zenye miinuko za nyanda za juu kaskazini mashariki.

Aidha, amesema kuwa katika kipindi cha msimu wa Juni hadi Agosti 2026, joto la bahari katika ukanda wa tropiki ya kati ya Bahari ya Pasifiki linatarajiwa kuwa juu ya wastani, hali inayoashiria kujijenga kwa hali ya El NiƱo.

Amesema kuwa kwa Bahari ya Hindi, joto la juu ya wastani linatarajiwa katika maeneo ya magharibi mwa bahari hiyo (pwani ya Afrika Mashariki) na joto la wastani linatarajiwa katika maeneo ya mashariki (pwani ya Indonesia).

Vilevile, upepo wa bahari wenye unyevunyevu uvumao kutoka mashariki unatarajiwa kuelekea katika maeneo ya ukanda wa pwani. Hali hii inatarajiwa kuongeza msukumo wa unyevunyevu kutoka baharini kuelekea nchini pamoja na kupunguza baridi ya wakati wa usiku kwa kuongeza kiwango cha chini cha joto na kusababisha mvua za nje ya msimu.

Kwa upande mwingine, joto la bahari katika eneo la kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi (kusini mwa Kisiwa cha Madagascar) linatarajiwa kuwa juu ya wastani. Hali hii inatarajiwa kudhoofisha mgandamizo mkubwa wa hewa katika eneo hilo na hivyo kupunguza kasi ya upepo wenye baridi kutoka kusini kuelekea katika maeneo ya nchi yetu.





Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...