Skip to main content

TMA YATOA ELIMU YA HALI YA HEWA KWA WAVUVI KUPITIA MRADI WA ECOFISH


Pemba, 20 Mei 2026

Mradi wa ECOFISH unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Denmark kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Shirika la Denmark la Maendeleo ya Kimataifa (DANIDA), unaendelea kuboresha shughuli za uvuvi kwa jamii ya Pwani na kuimarisha huduma za tahadhari za mapema za hali ya hewa nchini.

Katika utekelezaji wa mradi huo, wataalamu kutoka TMA walikutana na wavuvi pamoja na wakulima wa Mwani kwa lengo la kujionea hali halisi ya shughuli zao za kiuchumi na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa  wanazokabiliana nazo, sambamba na kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika shughuli za uvuvi na kilimo cha Mwani. Ziara hiyo iliambatana na semina maalum iliyowakutanisha wavuvi na wakulima wa Mwani ikiwa ni sehemu ya juhudi za mradi huo katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kufanya maamuzi sahihi na salama.

Akizungumza katika semina hiyo, Mtaalamu wa Hali ya Hewa kutoka TMA na msimamizi wa mradi, Dkt. Sarah Emerald Osima, alisema mradi wa ECOFISH una mchango mkubwa katika kuimarisha huduma za hali ya hewa na ustahimilivu wa jamii za Pwani kupitia tafiti, elimu na teknolojia za tahadhari za mapema.

Dkt. Sarah aliendelea kusema mradi huo pia umewezesha udhamini wa masomo kwa wanafunzi saba wa shahada za uzamili na uzamivu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IMS) pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambapo mmoja wao ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Alisema hatua hiyo inalenga kujenga wataalamu watakaosaidia sekta ya uvuvi na hali ya hewa kwa siku zijazo.

Aidha, wananchi wa kisiwani hapoo wamepongeza mradi huu wa ECOFISH na TMA kwa kuwapatia elimu hiyo, wakisema imewasaidia kuelewa na kutumia taarifa za hali ya hewa katika kupanga shughuli zao za uvuvi.

“Sasa tunajua umuhimu wa kutafuta na kutumia taarifa za hali ya hewa, jambo ambalo hapo awali tulikuwa tunalifanya kwa uelewa mdogo. Kwa sasa tumejifunza mambo mengi ikiwemo namna ya kutafsiri taarifa hizo kama zinavyotolewa na wataalamu,” alisema Afisa Uvuvi kutoka Wilaya ya Wete, Ndugu,Suleiman Ali Amadi.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...