Ayra Newstz
Siri iliyoficha ukewli juu ya kutoweka kwa Ramadhan Jafari maarufu @Muna, (47), eneo la Mbezi Luguruni, Ubungo, imebainika baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kukamilisha uchunguzi wa kina uliodumu kwa takribani wiki moja.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro leo Juni 23, 2026, Ramadhan Jafari aliyeripotiwa kupotea tarehe 16 Juni, 2026, amebainika kufariki dunia katika mazingira ya kusikitisha ndani ya makazi yake eneo la Kwembe.
SACP Muliro amesema taarifa ya kupotea kwa mzee huyo ilipokelewa na Kituo cha Polisi Kimara Gogoni na kuwashwa balaza la uchunguzi mara moja, huku wapelelezi kwa kushirikiana na wananchi walifanya ufuatiliaji wa nyumba hadi nyumba, simu hadi simu, hadi ukweli ulipopatikana.
Katika uchunguzi wa Jeshi la Polisi walimkamata kijana Juma Ramadhan maarufu @Juli, 21, ambaye ni mtoto wa marehemu, chanzo cha Polisi kinasema baada ya mahojiano ya kina, mtuhumiwa alieleza mwenendo wa tukio hilo.
Aidha, mtuhumiwa kwa sasa anashikiliwa huku uchunguzi ukiendelea kubaini sababu kamili zilizosababisha tukio hilo la kusikitisha.
Kamanda Muliro ametoa shukrani kwa wananchi kwa ushirikiano wao katika kutoa taarifa,huku akisisitiza kuwa hali ya usalama Dar es Salaam kwa ujumla ni nzuri na kwamba mkono wa sheria ni mrefu - mhalifu yeyote atakamata na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria bila kujali cheo au uhusiano.

Comments
Post a Comment