Skip to main content

KATIBU MKUU WA NISHATI ZAMBIA AIPONGEZA TANZANIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA UMEME


Aeleza Ushirikiano katika utekelezaji wa Mradi wa TAZA na faida zake Kikanda.

Asifu jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati nchini Zambia,  Mhe. Arnold Simwaba, amesema kuwa Tanzania na Zambia zimeendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa TAZA (Tanzania–Zambia Power Interconnection Project), wenye lengo la kuunganisha gridi za umeme za nchi hizo mbili kwa manufaa ya pande zote.

Mhe. Simwaba ameyasema hayo Juni 25, 2026, mkoani Dodoma, wakati wa kikao cha pamoja kilichowakutanisha wajumbe kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wizara ya Nishati ya Zambia, Mamlaka ya Umeme Vijijini ya Zambia pamoja na Shirika la Umeme Zambia (ZESCO), kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kuboresha huduma za umeme.

Ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika sekta ya umeme baada ya miradi mingi ya umeme kukamilika nchini. Aidha, amesifu  jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi  hususani matumizi ya umeme katika shughuli za kupikia.

Mhe. Simwaba amesema ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania katika sekta ya nishati utasaidia kuboresha upatikanaji wa umeme na kuharakisha matumizi ya nishati safi kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

“Mkutano huu ni muhimu kwetu kwa sababu tumekuja kujifunza na kubadilishana uzoefu. Tanzania inafanya kazi kubwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme, lakini pia katika utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia. Kwa upande wetu, mbinu tunazotumia Zambia katika kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya nishati safi zina tofauti kidogo. Ndiyo maana tumekuja kujifunza kutokana na mafanikio yenu,” alisema Mhe. Simwaba.

Kwa upande wake, Meneja wa Miradi ya Usambazaji Umeme wa TANESCO, Bw. Christopher Mbwija, amesema Tanzania na Zambia zinaendelea kushirikiana katika utekelezaji wa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme kati ya Tanzania na Zambia (TAZA), ambao ukikamilika utakuwa na mchango mkubwa katika kurahisisha biashara ya umeme kikanda.

Amesema mradi huo utaimarisha uhusiano wa mifumo ya umeme kati ya Kanda ya Afrika Mashariki na Kanda ya Kusini mwa Afrika kupitia jumuiya za East African Power Pool (EAPP) na Southern African Power Pool (SAPP), hivyo kuongeza fursa za biashara ya umeme na kuimarisha usalama wa nishati katika ukanda huo.

Ugeni huo kutoka Wizara ya Nishati ya Zambia, Mamlaka ya Umeme Vijijini ya Zambia na Shirika la Umeme Zambia (ZESCO) ulifanya ziara rasmi nchini kuanzia Juni 21, 2026, ambapo ulitembelea taasisi mbalimbali za sekta ya nishati nchini Tanzania, zikiwemo Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na TANESCO.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...