Skip to main content

MAMBO ALIA NA SERIKALI, AWAITA VIJANA AGUST 12

 


Na Ayra Newstz 

Mratibu wa Jukwaa la Vijana Taifa la Chama cha Ukombozi wa Umma(JUVICHA), Masoud Mambo, amesema kuwa Serikali imeshindwa kutengeneza mazingira rafiki kwa vijana na badala yake imekuwa ikiweka vikwazo vikubwa katika ukuaji wa uchumi wa vijana wa Kitanzania kwa kushindwa kuona thamani kubwa ya vijana katika ukuaji wa uchumi. 

Amesema hayo, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CHAUMA, ambapo ameeleza vijana ndio soko kubwa kutokana na uzalishaji mkubwa wanaoufanya, lakini pamoja na umuhimu huo wa vijana katika uzalishaji na ukuaji wa uchumi wa taifa, bado wamekuwa wakikumbana na changamoto lukuki, kama ambavyo vyama vya siasa, taasisi na makundi mbalimbali vimekuwa vikiwasemea.

Amesema kumekuwepo na sheria, sera na taratibu kadhaa ambazo kimsingi 7zinamnyima kijana nafasi ya kukua kiuchumi na kupata fursa ya kuingia katika ushindani wa soko la kimataifa.

Aidha, amesema kuwa vijana wa Kitanzania wanakumbwa na changamoto ya ukosefu wa ajira na kupanda kwa gharama za maisha, kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana, Tanzania kati ya vijana milioni moja wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka,. 

"Vijana laki mbili tu ndio huajiriwa kwenye sekta rasmi za umma na binafsi, sawa na asilimia 20, huku vijana laki nane (800,000) waliobaki, sawa na asilimia 80, huingia kwenye sekta zisizo rasmi kama vile kuendesha bodaboda, mama na baba lishe, kuuza matunda, mboga mboga na karanga"

Aidha, amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kupitia bajeti kuu iliyosomwa bungeni jijini Dodoma imeongeza gharama za usajili kwa vyombo vya usafiri, ikiwemo bodaboda, kutoka shilingi elfu tisini na tano (95,000) hadi laki moja na elfu hamsini (150,000), hatua ambayo imetajwa kuwa ni kuwadidimiza vijana kiuchumi.

Aidha, amesema kuwa bajeti hiyo pia haijaonesha mkakati wowote wa kutatua changamoto za vijana kutokana na kwamba Serikali imeshindwa kujenga uchumi unaoweza kutengeneza ajira kwa vijana na badala yake imekuwa ikiendelea kutoa mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kama suluhu ya ajira.

Katika hatua nyingine, Mambo amesema kuwa Agosti 12 mwaka huu vijana wa CHAUMA wataungana na vijana wote duniani katika kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani, ambayo ni siku muhimu ya kuongeza uelewa mpana juu ya mchango na changamoto zinazowakabili vijana duniani, maendeleo ya vijana kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuhamasisha ushiriki wa vijana katika kufanya maamuzi ya maendeleo, pamoja na kukuza amani, maendeleo na ushirikiano kati ya vijana wa mataifa mbalimbali.

"Uongozi wa Jukwaa la Vijana la Chama cha Ukombozi wa Umma (JUVICHA) umeamua kushiriki maadhimisho haya yatakayofanyika jijini Dar es Salaam tukiwa na kaulimbiu yetu, "Vijana Wakati ni Sasa" ikiwa na lengo la kuhamasisha vijana kuchukua hatua zitakazotengeneza kesho yao iliyo bora na vizazi vijavyo."

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...