Skip to main content

MD TWANGE ATOA RAI KWA MAMENEJA TANESCO KUONGEZA KASI YA KUPAMBANA NA WIZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME


Afungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mameneja na Wakurugenzi wa Kanda, Dodoma

Asisitiza umuhimu wa kuongeza ubunifu katika ukusanyaji wa mapato.

Awapongeza kwa kazi nzuri na kuendelea kuimarisha mahusiano na wadau

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, ametoa rai kwa mameneja wa TANESCO nchini kusimamia na kupambana kwa nguvu zote na changamoto ya wizi wa miundombinu ya umeme, ambayo imekuwa ikijitokeza katika maeneo mbalimbali ya mikoa wanayoisimamia.

Bw. Twange ameyasema hayo Juni 24, 2026, mkoani Dodoma wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa Mameneja na Wakurugenzi wa Kanda, wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Shirika pamoja na Kurugenzi ya Usambazaji.

Licha ya kuwapongeza mameneja hao kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuwahudumia wananchi, amesema kuna haja ya kila mmoja kuona uchungu wa mali za Shirika kwa kuongeza jitihada za kuhakikisha changamoto ya wizi wa miundombinu ya umeme inatokomezwa.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya. Mara nyingi tunapongezwa kwa utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Sasa ongezeni kasi ya kuhakikisha mali za Shirika zinalindwa. Pambaneni na changamoto ya wizi wa vifaa vya umeme, kwani matukio kama haya hayaleti taswira nzuri kwa Shirika,” alisisitiza Bw. Twange.


Katika Mkutano huo , Bw. Twange pia ameeleza umuhimu wa kuongeza ubunifu katika ukusanyaji wa mapato, akibainisha kuwa shughuli nyingi zinazofanywa na Shirika katika kuwahudumia wananchi hutegemea mapato yanayokusanywa.

Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Manyara, Mha. Regina MVungi amesema Mkutano huo unekuwa na mchango mkubwa katika kutathmini utendaji kazi pamoja na utekelezaji wa mpango mkakati wa Shirika. Huku Meneja wa TANESCO Ruvuma Mha. Eliseus Mhelela ameeleza namna walivyojipanga kuyafanyia kazi maelekezo  yaliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji ili kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi.

Mkutano huo wa Mameneja na Wakurugenzi wa Kanda,  umewashirikisha pia Mameneja Wakuu wa Kampuni Tanzu za TANESCO, umeanza rasmi Juni 24, 2026, na unatarajiwa kuhitimishwa Juni 26, 2026.


Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...