Skip to main content

MSUVA AUNGA MKONO MPANGO WA MAFUNZO WA JAB KUELEKEA AFCON 2027




Na Mwandishi Wetu

Mchezaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Simon Msuva, amepongeza mpango wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) wa kuandaa mafunzo maalum kwa Waandishi wa Habari kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), akisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha mchango wa sekta ya habari katika kuitangaza Tanzania, kukuza vipaji vya wanamichezo na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo zitakazotokana na mashindano hayo.

Msuva ametoa pongezi hizo leo, tarehe 19 Juni 2026, alipotembelea Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari zilizopo Posta Mpya, Mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula.

Amesema Waandishi wa Habari wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo nchini kwa kutangaza vipaji vya wanamichezo, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo na kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi.

“Mimi nawaombea waweze kutengeneza elimu ya kutosha kwa Waandishi wa Habari kwa sababu hawa Waandishi wa Habari wametufanya sisi tuinuke. Bila wao leo hii huenda nisingefahamika kama Simon Msuva. Wana nafasi kubwa sana katika nchi yetu, lakini pia wanahitaji kuendelea kupata elimu na mafunzo yatakayowasaidia kuwa bora zaidi katika kazi yao,” amesema Msuva.

Msuva amesema AFCON 2027 ni zaidi ya mashindano ya mpira wa miguu kwani yatatoa fursa katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, utalii, uwekezaji na ajira, hivyo kuna umuhimu wa Waandishi wa Habari kuandaliwa mapema ili waweze kuripoti kwa weledi na kusaidia wananchi kuelewa na kutumia fursa zitakazojitokeza.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, amemshukuru Msuva kwa kutembelea Bodi hiyo na kuunga mkono juhudi za kuimarisha taaluma ya habari kuelekea AFCON 2027.

Amesema JAB imeanza maandalizi ya mafunzo maalum kwa Waandishi wa Habari za michezo na kada nyingine za habari kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuripoti mashindano hayo kwa viwango vya kimataifa pamoja na kuibua na kuhabarisha umma kuhusu fursa za maendeleo zitakazotokana na AFCON 2027.

Wakili Kipangula amesema kupitia mafunzo hayo, Waandishi wa Habari watawezeshwa kuelewa kwa kina mchango wa michezo katika maendeleo ya taifa, uchumi wa michezo, utalii, uwekezaji na maeneo mengine muhimu yatakayochochewa na mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.

Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027, hatua inayofungua fursa kubwa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...