Skip to main content

NDEJEMBI ATAKA KASI YA UTENDAJI KAZI WA WIZARA YA NISHATI NA TAASISI KUONGEZEKA






Lengo ni kukidhi matarajio ya wananchi katika Sekta ya Nishati

 Dodoma

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewataka watendaji na watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake  kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao katika mwaka  mpya wa fedha 2026/2027 ili  kuweza kukidhi matarajio makubwa ya wananchi katika sekta ya nishati.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo katika kikao kazi kilichojumuisha viongozi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kilicholenga kupata matokeo ya tathmini ya utendaji kazi wa Wizara na taasisi hizo.

Kikao kazi hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba na  Makatibu Wakuu, Mhandisi Felchesmi Mramba na Dkt.James Mataragio.

Waziri Ndejembi amesema wananchi wanamatarajio mbalimbali ikiwemo kupata  umeme wa uhakika, kuongezeka kwa uzalishaji na matumizi ya gesi asilia na mafuta, uhakika wa upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na nishati safi ya kupikia 

 "Mwaka wa fedha unaokuja twendeni tukachape kazi, Watanzania wanamatarajio makubwa sana. Wana matarajio ya kuwa na umeme wa uhakika, wana matarajio ya kuona gesi ikiongeza uzalishaji, wana matarajio ya kuona vitalu vyetu vinapata wawekezaji, na vile ambavyo vina wawekezaji basi wanachimba. Wana matarajio ya kuona kwamba mafuta hayaishi ndani ya Tanzania." Amesema Mhe. Ndejembi

Aidha, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ana imani kubwa na Wizara ya Nishati, jambo linalodhihirishwa na kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ya nishati nchini.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...