Skip to main content

SEMU AIPINGA BAJETI KUU YA SERIKALI, ATOA HOJA HIZI..


Ayra Nwestz 

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, amesema Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2026/27 imeshindwa kutoa majibu ya msingi kwa changamoto zinazowakabili Watanzania katika sekta muhimu za afya, kilimo na biashara.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha uchambuzi wa bajeti hiyo, Semu amesema kuwa watanzania walitarajia kuona utekelezaji wa ahadi mbalimbali zilizotolewa na Serikali kuhusu kuboresha huduma za afya, hususan mpango wa afya kwa wote, lakini hali halisi inaonesha kuwa gharama za matibabu zinaendelea kuwa mzigo mkubwa kwa wananchi.

Ameeleza kuwa gharama za vipimo na matibabu ya magonjwa sugu zimeendelea kuwa kubwa katika hospitali za umma, huku wananchi wakilazimika kulipia huduma ambazo awali zilitarajiwa kutolewa kwa urahisi zaidi. Kwa mujibu wake, bajeti hiyo haijaeleza namna itakavyopunguza gharama hizo wala kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wote.

Semu alihoji utekelezaji wa mfumo wa bima ya afya kwa wote, akidai kuwa mfumo uliopo haujafanikiwa kuwafikia wananchi wengi kama ilivyokusudiwa. Alisema takwimu zinaonesha kuwa idadi kubwa ya Watanzania bado hawapo katika mfumo wowote wa bima ya afya, jambo linalowalazimu kutumia fedha nyingi wanapougua.

Kwa mujibu wa ACT-Wazalendo, suluhisho la kudumu ni kuanzishwa kwa mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wote ambao utawezesha wananchi wote kuchangia kwa viwango vinavyolingana na uwezo wao, huku Serikali ikiwachangia wale wasiokuwa na uwezo wa kuchangia.

Amesema bajeti hiyo haijaweka mikakati ya kutosha ya kuimarisha uzalishaji wa mbolea ndani ya nchi ili kupunguza utegemezi wa bidhaa za nje na kuwasaidia wakulima kupata pembejeo kwa bei nafuu.

Aidha, Semu alieleza kuwa sekta ya kilimo imeendelea kutengewa fedha chache ukilinganisha na mahitaji yake, licha ya kuwa ndiyo sekta inayoajiri idadi kubwa ya Watanzania na kuchangia sehemu kubwa ya pato la taifa. Alibainisha kuwa fedha zinazotengwa mara nyingi hazipelekwi kwa kiwango kilichoidhinishwa, jambo linalozorotesha maendeleo ya sekta hiyo.

Kuhusu Bandari ya Dar es Salaam, kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo alisema bado kuna maswali mengi kuhusu matokeo ya uwekezaji uliofanywa pamoja na ushiriki wa kampuni ya DP World katika uendeshaji wa bandari hiyo.

Amesema licha ya Serikali kueleza kuwa kiwango cha mizigo inayopita bandarini kimeongezeka, bado kuna changamoto za ucheleweshaji wa mizigo, uhaba wa miundombinu na kuendelea kuwepo kwa msongamano wa shughuli zinazohusiana na usafirishaji wa makontena ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

ACT-Wazalendo pia imeitaka Serikali kuweka wazi mikataba ya uendeshaji wa bandari pamoja na faida halisi inayopatikana kutokana na uwekezaji huo ili wananchi waweze kujua manufaa yanayopatikana kutokana na rasilimali zao.

Kwa ujumla, Semu amesema Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/27 imeendelea kuongeza mzigo kwa wananchi wa kawaida kupitia kodi na tozo mbalimbali bila kutoa suluhisho la kudumu kwa changamoto za msingi zinazowakabili.

Amesisitiza kuwa ACT-Wazalendo itaendelea kupigania matumizi bora ya fedha za umma na kusukuma sera zitakazohakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania wote, hususan katika sekta za afya, kilimo, ajira na maendeleo ya uchumi.

Katika sekta ya afya, Semu pia alieleza kuwa bado kuna uhaba mkubwa wa watumishi wa afya, dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma. Alisema bajeti ya mwaka 2026/27 haijaonesha mkakati wa kutosha wa kuajiri watumishi wapya wala kuongeza upatikanaji wa dawa muhimu kwa wananchi.

Akizungumzia sekta ya kilimo, Semu amesema wakulima wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za mbolea pamoja na utegemezi mkubwa wa mbolea kutoka nje ya nchi, amedai kuwa zaidi ya asilimia 69 ya mbolea inayotumika nchini inaagizwa kutoka nje, hali inayochangia kupanda kwa gharama za uzalishaji.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...