Skip to main content

SERIKALI IMEDHAMIRIA KULETA MAPINDUZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA - NAIBU WAZIRI SALOME




Imepunguza kodi kwenye vifaa vya Nishati Safi.

Lengo ni kuwafikia wananchi wa aina zote.

Imeelezwa kuwa Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka dhamira  ya dhati  katika kuleta  mapinduzi ya matumizi ya Nishati  Safi ya kupikia yanayoongozwa na mkakati wa taifa wa Nishati Safi ya kupikia  kwa mwaka 2024-2034 unaolenga kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania wanatumia Nishati Safi ya kupikia ifikapo 2034.

Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Nishati  Mhe. Salome Makamba alipokuwa akifunga kongamano la kuhamasisha na kuelimisha juu ya matumizi ya Nishati  safi ya kupikia Juni 25, 2026 lilokuwa likifanyika katika Ukumbi  wa East  Africa Commercial Logistic Center uliopo Jijini  Dar es Salam.

Mhe. Salome amesema kuwa ni muda wa kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na matumizi ya Nishati Safi  ya Kupikia ili kuweza kulinda afya pamoja na kutunza Mazingira hali itakayosaidia Nchi kuingia kwenye mapinduzi  makubwa ya Matumizi ya Nishati  Safi.

"Katika kuhakikisha tunafikia lengo la asilimia 80 mwaka 2034 Serikali  imefanya maamuzi mbalimbali  ya kisera  na kiutendaji  ikiwa ni pamoja na kuondoa au kupunguza kodi mbalimbali kwenye vifaa vya Nishati safi ili kupunguza gharama ya vifaa hivyo kwa mtumiaji wa mwisho" alieleza Mhe. Salome.

Naye Meneja wa Masoko kutoka Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Fredrick Kalinga ameeleza kuwa TANESCO  imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha inawafikia wananchi wote kwa kuwaelimisha na kuwahamisisha juu ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwa umeme ili kuweza kutengeneza uchumi endelevu kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

"Tutaendelea kuhakikisha tunapata miradi ambayo itatuwezesha kusambaza majiko mengi zaidi kwa wananchi na wateja wetu ili wote tuweze kutumia Nishati Safi ya Kupikia kwa umeme ambayo sisi kama shirika tunazalisha na tunapenda wateja wetu waendelee kutumia"

Aliongeza kuwa tofauti na Nishati Safi ya kupikia kwa Umeme TANESCO  imeendelea kuimarika  kwa maana ya huduma kwa wateja kwa kuhakikisha wateja wote wanapata taarifa rasmi na sahihi wakati wote.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...