Skip to main content

KAPINGA AIPONGEZA NIDA


Waziri  wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, ameipongeza kampuni ya Nida kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora unaoendana na soko, huku akisisitiza kuwa wanatambua kazi kubwa inayofanywa na kampuni hiyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia. 

Waziri Kapinga ametembelea banda la Kiwanda cha NIDA katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo amesema ameridhishwa na ubora unaozalisha katika bidhaa. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Mahusiano wa NIDA, Mohamed Honelo, amesema kampuni hiyo, imejenga mnyororo kamili wa uzalishaji unaoanzia kwa kuwawezesha wakulima wa pamba, kununua mazao yao, kuyasindika kuwa nyuzi na vitambaa katika kiwanda chake kilichopo Mbeya, kisha kuvipeleka NIDA Textile Mills kwa ajili ya uchapishaji kabla ya kuviuza kupitia maduka yake.

Aidha, kampuni hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto ya ajira kwa kutoa ajira za moja kwa moja kati ya 1,500 na 2,000, pamoja na ajira za muda kulingana na mahitaji ya uzalishaji.


Sambamba na hilo, amesema mfumo huo unaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 inayolenga kuongeza viwanda nchini, kuzalisha ajira, kukuza biashara na kuongeza mchango wa sekta ya viwanda katika uchumi wa Taifa.

Hata hivyo, amesema kuwa bidhaa za kampuni hiyo, zikiwemo kanga, vitenge, mashuka na bidhaa nyingine zinazotokana na pamba, zinapatikana katika maduka ya NIDA na NIDA Textile Mills, huku akiwakaribisha wananchi kuzinunua na kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa nchini.

Aidha, Honelo aliiomba Serikali kuweka utaratibu utakaowezesha sehemu kubwa ya pamba inayozalishwa nchini kubaki kwa matumizi ya viwanda vya ndani badala ya kuuzwa nje kama malighafi.


“Tunaiomba Serikali iweke akiba ya pamba kwa ajili ya viwanda vya ndani. Ni kweli hatuwezi kununua pamba yote kwa wakati mmoja, lakini kiasi kinachobaki kihifadhiwe ili baadaye viwanda vya ndani viweze kukinunua badala ya kulazimika kuagiza au kununua pamba hiyo hiyo kwa gharama kubwa kutoka nje,”amesema Honelo.

Ameongeza kuwa, pia gharama kubwa za uzalishaji zinapunguza uwezo wa viwanda vya ndani kushindana na bidhaa kutoka nje, huku wazalishaji wa nchi nyingine wakinufaika na gharama ndogo za uzalishaji zinazowaruhusu kuuza bidhaa kwa bei nafuu zaidi.

"Naipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuhamasisha maendeleo ya sekta ya viwanda, akisema hatua hiyo itaongeza ajira, kukuza uchumi na kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye msingi imara wa viwanda"amesema



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...