Skip to main content

UBUNIFU WA BANDA WAIVUSHA TBA KWENYE TUZO ZA SABASABA



Ayra news 

Jitihada za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuonesha fursa za uwekezaji na miradi yake ya kimkakati katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), zimezaa matunda baada ya taasisi hiyo kutwaa tuzo ya mshindi wa pili katika kipengele cha Banda Bora upande wa Sekta ya Miliki na Real Estate.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa wakati wa sherehe za kufunga maonesho hayo zilizofanyika Julai 13, 2026, na kupokewa na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TBA,  Amina Lumuli, kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Arch. Daud W. Kondoro.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Lumuli alisema mafanikio hayo yanadhihirisha namna TBA ilivyoweza kutumia maonesho hayo kuwasogezea wananchi huduma, kutoa elimu kuhusu majukumu yake na kufungua milango ya fursa kwa wawekezaji kupitia miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP).

Alisema banda la TBA lilikuwa kivutio kwa wageni wengi waliotembelea maonesho hayo kutokana na maelezo kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini, ikiwemo ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, majengo ya taasisi za umma na kazi za ukarabati pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya michezo, ukiwemo Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa Bi. Lumuli, mwitikio wa wananchi na wadau umeongeza imani kwa TBA na kuthibitisha kuwa taasisi hiyo inaendelea kuwa miongoni mwa vinara wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi yenye viwango vya kitaalamu na mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

Alitoa wito kwa sekta binafsi na wawekezaji kutumia fursa zilizopo kushirikiana na TBA katika utekelezaji wa miradi ya ubia, akisema ushirikiano huo utasaidia kuongeza kasi ya maendeleo ya miundombinu na kuboresha huduma kwa wananchi.

Sherehe za kufunga Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba ziliongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambapo taasisi mbalimbali zilizofanya vizuri zilitunukiwa tuzo kwa kutambua ubunifu na mchango wao katika utoaji wa huduma kwa umma.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...