Skip to main content

UKAGUZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WAANZA SEPTEMBA


Dar es Salaam. Serikali imesema itaanza ukaguzi wa vyama vya ushirika nchini kuanzia Septemba mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha uwajibikaji, kuongeza imani ya wanachama na kuboresha utendaji wa sekta hiyo inayochangia zaidi ya Dola za Marekani bilioni mbili katika uchumi wa taifa.

Akizungumza katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Kamishna Mkuu wa Shirika la Wakaguzi na Wasimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Jeremia Jackson Mugeta, alisema taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha vyama vyote vya ushirika vinakaguliwa kwa wakati na kwa kuzingatia sheria.

Alisema vyama vya ushirika vinapaswa kuandaa na kuwasilisha taarifa zao za fedha kwa ofisi za shirika katika mikoa yote ya Tanzania Bara ili kurahisisha utekelezaji wa mpango wa ukaguzi wa mwaka wa fedha 2025/26.

"Tunataka wanachama wa vyama vya ushirika waendelee kuwa na imani na vyama vyao kwa kuhakikisha fedha zinatumika kwa uwazi na taarifa za ukaguzi zinapatikana kwa wakati," alisema.

Mugeta alisema hali ya usimamizi wa vyama vya ushirika imeendelea kuimarika, akibainisha kuwa idadi ya vyama vinavyopata hati safi za ukaguzi imeongezeka kutoka asilimia nne katika miaka ya nyuma hadi kufikia asilimia 16 kwa sasa.

Aidha, alisema vyama vinavyopata hati zenye mashaka vimepungua kwa kiasi kikubwa kutoka takribani asilimia 37 hadi asilimia tano, jambo alilosema linaonyesha kuongezeka kwa uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria za fedha.

Kwa mujibu wa Mugeta, pamoja na kufanya ukaguzi, taasisi hiyo inaendelea kutoa ushauri kwa viongozi wa vyama vya ushirika kuhusu usimamizi wa fedha, uandaaji wa taarifa za kifedha na uzingatiaji wa sheria na kanuni ili kuimarisha utendaji wa vyama hivyo.

Akizungumzia mchango wa sekta ya kilimo, alisema inaendelea kuwa mhimili wa uchumi wa Tanzania kwa kuchangia zaidi ya asilimia 26 ya Pato la Taifa, huku mazao yanayouzwa kupitia vyama vya ushirika yakichangia zaidi ya Dola za Marekani bilioni mbili.

Alisema Serikali itaendelea kuimarisha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo ili kuongeza ufanisi wa sekta ya ushirika na kuwahakikishia wakulima huduma bora zitakazoongeza tija na kipato chao.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...