Skip to main content

VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO YA ASILIMIA 10


Na Ayra Newstz 

Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wametoa wito kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuchangamkia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri, wakieleza kuwa fedha hizo zimeendelea kubadilisha maisha ya wananchi kwa kuwawezesha kuanzisha na kukuza biashara pamoja na viwanda vidogo.

Wito huo umetolewa walipotembelea Banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo pia walipongeza maandalizi ya maonesho hayo na ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa Tanzania.


Akizungumza katika maonesho hayo, kiongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amesema anaungana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, kuwapongeza waandaaji wa maonesho hayo kwa kufanikisha tukio hilo ambalo limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara, uwekezaji na ubunifu wa wazalishaji wa ndani.

Amesema ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa Tanzania umeongezeka kwa kiwango kikubwa na sasa zinaweza kushindana katika masoko mbalimbali kutokana na maboresho ya viwango vya uzalishaji.

Akitolea mfano bidhaa za ngozi na viatu vinavyozalishwa nchini, amesema vina ubora unaoweza kushindana na bidhaa nyingine katika maduka makubwa na masoko ya ndani na nje ya nchi.


Kuhusu mikopo ya asilimia 10, amesema utekelezaji wake umeleta mafanikio makubwa kwa vikundi mbalimbali ambavyo vimefanikiwa kuanzisha viwanda vidogo na kupanua shughuli zao za uzalishaji baada ya kunufaika na fedha hizo.

Amesema baadhi ya vikundi vimepokea mikopo inayofikia zaidi ya Sh milioni 80 na vingine zaidi ya Sh milioni 30, hali ambayo imechangia kukuza uchumi wa wananchi na kuongeza ajira.

"Tumeshuhudia vikundi vimeanzisha mpaka viwanda vidogo vidogo baada ya kupata mikopo hii. Hii inaonyesha fedha hizi zina matokeo chanya na zinaendelea kubadilisha maisha ya wananchi," amesema.


Ameongeza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam itaendelea kutenga na kutoa mikopo hiyo kupitia maamuzi ya Baraza la Madiwani ili kuhakikisha makundi yanayolengwa yanaendelea kunufaika.

Aidha, amesema halmashauri imeimarisha mfumo wa usimamizi wa mikopo hiyo kwa kushirikiana na taasisi za kifedha ili kuhakikisha fedha zinarejeshwa kwa wakati na kuwafikia wanufaika wengi zaidi.

Amesema katika maonesho hayo pia kuna dawati maalumu la utoaji elimu kwa wananchi kuhusu utaratibu wa kuomba, kupata na kurejesha mikopo hiyo ili kuongeza uelewa na ushiriki wa wananchi.


Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetenga zaidi ya Sh bilioni 22 kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, huku ikiendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuboresha mazingira ya biashara kwa kutenga fedha za ujenzi wa miundombinu ya wajasiriamali

Amesema fedha hizo zitaelekezwa katika ujenzi wa maeneo ya uzalishaji, viwanda vidogo na masoko ya kisasa yatakayowawezesha wajasiriamali kuongeza thamani ya bidhaa zao na kupata masoko yenye uhakika

Amewataka wananchi kutembelea Banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Maonesho ya Sabasaba ili kupata elimu kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na halmashauri pamoja na kujionea mafanikio ya vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Elihuruma Mabelya amesema Jiji limetumia Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) kujifunza mbinu zitakazosaidia kuboresha utoaji wa huduma za ardhi, kupunguza migogoro ya umiliki na kurahisisha upatikanaji wa hati kwa wananchi.

Amesema kuwa, kupitia ziara hiyo imewapa viongozi nafasi ya kujionea huduma zinazotolewa na Wizara ya Ardhi pamoja na kazi inayofanywa na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kuwahudumia wananchi.

Mabelya amesema kupitia banda hilo wamejifunza umuhimu wa kuwa na kituo cha pamoja cha utoaji wa huduma za ardhi kitakachorahisisha upatikanaji wa hati, leseni za makazi, ulipaji wa kodi ya ardhi pamoja na huduma nyingine zinazohusu sekta hiyo.

"Kituo cha pamoja cha huduma za ardhi kinaweza kutusaidia kupunguza malalamiko ya wananchi na changamoto wanazokutana nazo katika utoaji wa hati, leseni za makazi na huduma nyingine za ardhi," amesema.

Amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam itatumia mafunzo yaliyopatikana katika maonesho hayo kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi katika kushughulikia masuala ya ardhi.


Naye, Meya wa jiji la Dar es Salaam Nurdin Bilal amesema mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu imeanza kuonesha matokeo baada ya baadhi ya wanufaika kutumia fedha hizo kuanzisha viwanda vidogo na kupanua uzalishaji wa bidhaa.

Bilal amesema baadhi ya vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo vimeweza kupiga hatua kubwa kiuchumi, huku vingine vikifikia hatua ya kuanzisha viwanda vidogo baada ya kupata fedha za kuwawezesha kuongeza uzalishaji.

"Tumeshuhudia kuna vikundi pale vimeanzisha mpaka viwanda vidogo vidogo na vimepata zaidi ya Sh milioni 80 za kuendelea. Wengine wamepata milioni 30 na huu ni mfano tu, wapo wengi wa aina hiyo,"aamesema.

Hata hivyo, amesema mafanikio hayo yanaonesha kuwa mikopo hiyo si suala la maneno pekee bali ni chachu ya kuwawezesha wananchi kujenga shughuli zao za kiuchumi.



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...