Skip to main content

VITUMBUA FESTIVAL YAZINDULIWA, WASHINDI KUNUFAIKA NA KIWANJA NA FEDHA TASLIMU


Ayra Newstz 

Umoja wa Mama na Baba Lishe Tanzania (UMALITA) umetangaza kuanzisha tamasha jipya la Vitumbua Festival, litakalofanyika Julai 30, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuinua hadhi ya wachoma vitumbua, kuongeza thamani ya biashara hiyo na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa UMALITA Taifa, Avijawa Omary  alisema tamasha hilo litawakutanisha wachoma vitumbua kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam katika mashindano yatakayolenga kutambua ubunifu na kuwapa motisha wajasiriamali hao.


Alisema mshindi wa kwanza atajishindia fedha taslimu, kiwanja pamoja na eneo maalumu la kufanyia biashara ya vitumbua, huku washindi wa pili na wa tatu wakipatiwa fedha taslimu, vifaa vya biashara na zawadi nyingine mbalimbali.

"Tunataka kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu biashara ya vitumbua kwa kutambua mchango wake katika kukuza uchumi wa familia, kuajiri vijana na wanawake pamoja na kuchochea maendeleo ya sekta ya ujasiriamali," alisema Avijawa.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UMALITA, Johajulieth Madata, alisema tamasha hilo pia litatumika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambapo washiriki wote watapatiwa elimu kuhusu matumizi ya gesi ya kupikia (LPG).

Alieleza kuwa matumizi ya gesi badala ya kuni na mkaa yatasaidia kulinda mazingira, kuboresha afya za wachoma vitumbua, kuongeza usafi katika maandalizi ya chakula na kuinua tija ya biashara zao.


Aidha, baadhi ya wajasiriamali wanaojishughulisha na biashara ya vitumbua wameeleza matumaini yao kuwa tamasha hilo litakuwa chachu ya kutangaza bidhaa zao, kuwafungulia masoko mapya na kuboresha mazingira ya kazi pamoja na kipato chao.

Tamasha hilo linatarajiwa kuanza saa 12:00 asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, likiwa na shughuli mbalimbali za burudani, elimu na mashindano yatakayoshirikisha wachoma vitumbua kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam.


Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...