Skip to main content

TFS YAWAPA ELIMU WACHONGAJI VINYAGO MWENGE



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umewapa elimu wafanyabiashara na wachongaji wa vinyago katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam kuhusu sheria, kanuni na taratibu za uvunaji, usafirishaji na biashara ya mazao ya misitu, ikiwemo namna ya kusafirisha bidhaa hizo nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo jana, Agosti 12, 2026, Mhifadhi wa Misitu wa TFS Wilaya za Kinondoni na Ubungo, Dotto Ndumbikwa, alisema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wafanyabiashara kuelewa taratibu zinazotakiwa, kufanya biashara zao kwa ufanisi na kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kutofuata sheria.

Ndumbikwa alisema TFS imeambatana na wahifadhi kutoka Kanda ya Mashariki, wakiwemo wanaosimamia shughuli za misitu katika eneo la Uwanja wa Ndege, kwa lengo la kusikiliza changamoto za wafanyabiashara na kuzitafutia ufumbuzi. “Tunapokaa kuwasikiliza na kuwapa elimu, inawasaidia wao kuendelea na biashara zao vizuri bila kupata matatizo,” alisema.

Aliwataka wafanyabiashara wa mazao ya misitu kufika katika ofisi husika za Serikali kabla ya kuanza biashara ili kupata elimu kuhusu taratibu, vibali na tozo zinazohitajika. Pia aliwataka kuwa makini wakati wa ukaguzi wa bidhaa zao, hususan viwanja vya ndege, kwa kuhakikisha afisa anayefanya ukaguzi anajitambulisha na kuonyesha kitambulisho cha kazi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA), Sebastian Daniel Mbebe, alisema elimu hiyo imewasaidia kuelewa sheria na taratibu ambazo awali zilikuwa chanzo cha changamoto, akisema wachongaji nao wamebaini baadhi ya maeneo ambayo hawakuwa wakifuata ipasavyo, ikiwemo kuwa na vibali vinavyotakiwa. “Hata sisi upande wetu kama uchongaji tulikuwa na makosa. Kuna vibali vingi tulikuwa hatuvitekelezi kwa mujibu wa sheria inavyotakiwa, lakini leo tumepata elimu na tumejua tunachotakiwa kufanya,” alisema.

Hata hivyo, Mbebe alisema bado kuna changamoto ya tozo wanazoziona kuwa kubwa, hasa kwa vinyago vya twiga, faru, simba na tembo ambavyo vinaweza kuwa na uzito mkubwa licha ya kuwa tayari ni bidhaa za sanaa. Alisema hali hiyo inaweza kuongeza gharama kwa wateja wanaosafirisha bidhaa hizo kupitia viwanja vya ndege, huku akieleza kuwa wataendelea kufuata taratibu na kulipia vibali vinavyohitajika wakati wakisubiri hatua zaidi kuhusu mapitio ya tozo hizo.

Naye mdau wa mazao ya misitu, Mwanne Mashugu, aliishukuru TFS kwa kuwafikia katika eneo lao la biashara na kuwapa elimu kuhusu taratibu kuanzia kupata mazao hadi kuyafikisha madukani, pamoja na namna ya kulipia tozo na kupata vibali vya usafirishaji. “Kwa elimu tuliyopewa tutaweza kuwaelimisha wateja wetu na kuwasaidia kufanikiwa kupita na mizigo yao salama bila mizigo yao kubaki pale uwanja wa ndege,” alisema.

TFS imeendelea kuwasisitiza wafanyabiashara na wadau wa mazao ya misitu kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa, huku ikiwataka kupata elimu na vibali kutoka katika ofisi husika za Serikali kabla ya kuanza biashara au kusafirisha bidhaa hizo nje ya nchi.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...