Skip to main content

Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24,zijazo kuanzia leo Agust 18,2026


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 kuanzia saa 3:00 usiku wa Agosti 18, 2026, ikieleza kuwa baadhi ya maeneo nchini yanatarajiwa kukumbwa na mawimbi kiasi, mvua na ngurumo pamoja na vipindi vya jua.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika mikoa ya Kagera, Mara na Simiyu, kunatarajiwa hali ya mawimbi kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.

TMA imesema katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, hali ya mawimbi kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua inatarajiwa.

Kwa upande wa Zanzibar, ikiwemo Unguja na Pemba, pamoja na mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi, Mwanza, Geita na Shinyanga, Manyara, Dodoma na Singida, mvua pamoja na mawimbi kiasi na vipindi vya jua vinatarajiwa.

Hali kama hiyo inatarajiwa pia katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi na Mtwara, pamoja na Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe na Songwe.

Katika taarifa hiyo, TMA imeeleza kuwa kwa Pwani, kuanzia Kusi kwenda Kaskazini Mashariki hadi Kusi, kutakuwa na upepo unaotarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa.

Aidha, hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi, hivyo wananchi wanaofanya shughuli za baharini wametakiwa kuzingatia taarifa za hali ya hewa na kuchukua tahadhari.

Kwa upande wa joto, TMA imesema miji ya Tabora na Kigoma inatarajiwa kuwa miongoni mwa maeneo yenye viwango vya juu vya joto, ambapo Tabora inatarajiwa kufikia nyuzi joto 31 za Selsiasi, huku Kigoma ikifikia nyuzi joto 30.

Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Zanzibar zinatarajiwa kufikia nyuzi joto 29, huku Arusha na Njombe zikitarajiwa kuwa na joto la chini zaidi, likifikia nyuzi joto 23.

TMA pia imetoa matarajio ya hali ya hewa kwa siku ya Alhamisi, Agosti 20, 2026, ikisema vipindi vya hali ya baridi vinatarajiwa kupungua katika maeneo mengi ya nchi.

Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa zinazotolewa mara kwa mara na kuchukua tahadhari kulingana na hali inayotabiriwa katika maeneo yao.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...